Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Wednesday, 9 August 2017

Waziri Mkuu apiga marufuku

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema kuanzia sasa ni marufuku kuweka bei ya tumbaku kwa dola za Marekani kwa sababu imechangia kuwaumiza wakulima wa zao hilo.

Amesema wanunuzi wa zao hilo wana uhuru wa kuweka bei zao kwa dola lakini bei hiyo itafsiriwe kwa shilingi za Kitanzania ili wakulima waweze kutambua bei elekezi tangu mwanzo wa msimu.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo jioni (Jumatano, Agosti 9, 2017) wakati akizungumza na wadau wa zao la tumbaku zaidi ya 600 wakiwemo wabunge, viongozi wa dini, chama na Serikali kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Isike-Mwanakiyungi, mjini Tabora.

Hivi sasa bei elekezi kwa msimu huu wa tumbaku ni dola mbili za Marekani kwa kilo moja ya tumbaku sawa na sh. 4,400 hadi sh. 4,500 za Tanzania.

"Kwa mfano, mkulima anapouza tumbaku anaambiwa kilo zake zina thamani ya dola za marekani 90. Wakati anapokuja kulipwa bei ya shilingi inakuwa imebadilika, kwa hiyo kama aliuziwa wakati thamani ya dola moja ikiwa ni sh. 1,500/- na wakati wa kulipwa imefikia sh. 2,000/- hatalipwa kwa bei ya sasa. Bali atalipwa kwa bei ileile ya zamani jambo ambalo linamuumiza mkulima," amesema Waziri Mkuu

CHANZO: EAST AFRICA TV(EATV)

No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post