Mbunge wa jimbo la Kigoma Ujiji Mh. Zitto Kabwe amekingia kifua kauli inayotolewa na serikali ikiwashutumu vyama vya upinzani kushiriki na kutoa taarifa za ndege kuzuiliwa nchini Uingereza, na kusema kuwa kama wananchi wana kila haki ya kuhoji.
Mh. Zitto Kabwe
Akijibizana na baadhi ya wananchi kwenye ukurasa wake wa twitter, Zitto Kabwe ameandika akisema suala kama hilo ni lazima watu wahoji, na sio kama hawapendi maendeleo yanayofanywa na uongozi wa Rais Magufuli, isipokuwa wanataka serikali ifanye vitu kwa uhakika zaidi, ili kuepusha kujiingiza kwenye hasara na migogoro kama hiyo.
“Watu ni lazima wahoji mtake mistake, hakuna anayetaka msubiri, tunataka mfanye Kwa uhakika, tutaendelea kuhoji na lazima serikali ijibu”, aliandika Zitto Kabwe.
Mh. Zitto Kabwe aliendelea kuandika “hatukutaka mnunue ndege hovyo hovyo, lakini ndege tunataka na tunapanda, mkihojiwa mnaleta viroja, jibuni hoja tu viroja vya nini ?”, aliandika Zitto Kabwe.
Siku ya tar 18 Agosti Mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu Anthipas Lissu, alitoa taarifa kuwa kuna mali za Tanzania zimezuiliwa nchini Canada kutokana na deni ambalo serikali inadaiwa na kampuni ya ukandarasi.
Baada ya taarifa hizo kutolewa na mbunge huyo, serikali ikathibitisha uwepo wa suala hilo na kuongeza kuwa kuna ya watu wa vyama vya upinzani wameshirikiana na makampuni ya nje kufungua kesi kama hizo, ili kuweka vikwazo kwa serikali kuweza kufanikisha mipango ya maendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya tano
No comments:
Post a Comment