Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Monday, 7 August 2017

WABUNGE WA CHADEMA WAITWA POLISI NA KUZUIWA KWA UCHOCHEZI NA UHAMASISHAJI KILIMO CHA BANGI

Wabunge (2) wawili wa CHADEMA huko Tarime Mara wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.

John Heche (MB) Tarime Vijijini na Esther Matiko (MB) Tarime Mjini. Wote kwa pamoja wanazuiliwa kituo cha Polisi cha Kanda maalum Tarime na Rorya.

Wabunge hao wamefika kituoni hapo kuitikia wito wa RCO wa Kanda maalumu hiyo ya Tarime-Rorya.

John Heche anatuhumiwa kwa uchochezi wa wananchi kuchukua hatua juu ya wizi wa MGODI WA ACCACIA WA NYAMONGO kama ulivyobainishwa na Rais Magufuli kwa kamati zake mbili za makinikia.

Naye  Esther Matiko anazuiliwa kwa tuhuma za kuhamasisha kilimo cha Bangi. Mhe.Esther Matiko aliwaahidi wananchi wa Tarime kuwa atapeleka Muswada Bungeni wa kujadiri manufaa na madhara ya kilimo cha Bangi.

Kwa sasa wote wako ofisini kwa RCO na mahojiano yanaendelea.


No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post