Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Wednesday, 9 August 2017

KOREA LASKAZINI IMESEMA KWAMBA INATAFAKARI MPANGO WA

Korea Kaskazini imesema kwamba inatafakari mpango wa kurusha makombora ya masafa ya kati na mbali karibu na Guam, eneo ambalo Marekani huwa na ndege zake za kuangusha mabomu saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuitishia Pyongyang kwamba itakabiliwa kwa "moto na ghadhabu" baada ya vyombo vya habari kuripoti kuwa Korea Kaskazini imeweza kuunda kichwa cha silaha cha nyuklia chenye uwezo wa kutosha kwenye makombora yake.

Kisiwa cha Guam kina ukubwa wa kilomita mraba 541 na kinapatikana bahari ya Pasifiki kati ya Ufilipino na Hawaii.
Majibizano kati ya Marekani na Korea Kaskazini yamezidi baada ya Pyongyang kufanyia majaribio makombora mawili yenye uwezo wa kusafiri kutoka bara moja hadi nyingine, na kudai kwamba sasa ina makombora yanayoweza kufika Marekani bara.
(Picha:Reuters)

No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post