Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Saturday, 12 August 2017

MBUNGE MTEULE WA VITI MAALUM (CUF) "ALONGA"AELEZEA VIPAUMBELE VYAKE.

Mbunge mteule wa viti maalum (CUF) wa jimbo la Handeni ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa.  mbunge amesema kuwa atautumia muda wake kama mbunge kuwatumikia vyema wananchi wa jimbo lake.

Akizungumza na mwandishi wetu Bi Magogo amekishukuru chama chake cha CUF kumwamini na kumpa dhamana ya kukiwakilisha bungeni kuwatumikia wananchi wa jimbo la Handeni.

"Chama kimenipa dhamana ya kukiwakilisha na kuuwakilisha mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla wakiwemo wananchi bungeni hivyo nitawatumikia wana Handeni hasa kutatua changamoto ya maji wamama Wa handeni wanalalamika sana na wengi wanahatarisha mpaka ndoa zao kwa sababu ya maji na hata uchumi wao kudorora hivyo nitahakikisha nashirikiana nao kupunguza tatizo la maji katika jumbo la handeni na sambamba kuwasaidia wakulima Wa Handeni kuwa na upeo Wa masoko ya bidhaa zao kwani wengi wanalima lakini bidhaa zao hukosa elimu stahiki ya masoko ya mazao wanayolima "alisema Bi SONIA MAGOGO.

Kuhusu suala la migogoro ya ardhi Bi Magogo amesema kuwa suala hilo ni changamoto kwani ardhi kubwa iko mikononi mwa watu wachache hivyo atatumia kiti chake cha Ubunge kuyasemea masuala ya ardhi bungeni ili wanahandeni wanufaike na ardhi yao kwa maendeleo ya uchumi.

Kuhusu tabia za baadhi ya wabunge Wa vyama vya upinzani kususia baadhi ya mambo bungeni na kutoka nje Bi Magogo amesema siyo busara kwa wabunge hao kutoka nje ya bunge bali wanatakiwa kuangalia wanapingana vipi na hoja zilizo mbele yao kwani hoja hupingwa kwa hoja na si kuikimbia hoja kwani wanawanyima wananchi wao fursa ya kuweza kutatuliwa matatizo yao kwani huwezi kuwasemea wananchi ukiwa nje ya bunge.

Hata hivyo amewataka wananchi wa Handeni kumpa ushirikiano huku na kuahidi kuwa nao bega kwa bega wakiijenga vizuri Handeni yenye fursa mbambali za uwekezaji kwa wazawa na wageni na kuitekeleza vizuri Sera ya Tanzania ya viwanda bila kujali itikadi za vyama vyao na kuifanya Handeni kuwa sehemu ya Tanzania yenye viwanda.



No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post