Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Thursday, 10 August 2017

JESHI LA KOREA KASKAZINI LIMESEMA LIMEKAMILISHA MPANGO WA KUSHAMBULIA KISIWA CHA GUAM

Jeshi la Korea Kaskazini limesema kwamba limekamilisha mpango wa kushambulia kisiwa cha Marekani cha Guam kwa kutumia kombora, na hivi sasa linasubiri tu mpango huo kuidhinishwa na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un.

Kim Rak Gyom, kamanda wa jeshi la Korea Kaskazini alinukuliwa na shirika la utangazaji la Korea (Korean Central News Agency) akisema kwamba kikosi chake kiko katika harakati za mwisho wa kuandaa mpango wa kushambulia kisiwa cha Guam ambacho kiko katika bahari la Pacific. Gyom alisema kwamba watatupa kombora aina ya Hwasong-12 kupitia anga za Japan na kuangusha kambora hilo kama kilomita 30 kwenye maji karibu na kisiwa cha Guam kilichoko karibu kilomita 3,356.7  kutoka Korea Kaskazini.

Amri ya kuandaliwa kwa shambilizi hilo lilitolewa na Kim Jong Un kama onyo kwa Marekani na jeshi lake.  "Korea Kaskazini inaonya Marekani kwamba tunazidi kukerwa na vitisho vyake vya kutushambulia na vikwazo vya kila mara dhidi yetu," Gyom alisema.

No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post