Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kusema anataka watu wanaokula rushwa wengi wao wafungwe kwani watu hao wanasababisha watu wakose barabara, madawa na kukosa maendeleo kutokana na watu kula rushwa.
Rais John Pombe Magufuli.
Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akimuapisha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali, John Julius Mbungo leo Ikulu jijini Dar es Salaam na kumtaka afanye kazi kuhakikisha rushwa inakomeshwa.
"Umepewa hilo jukumu kalisimamie na tunaimani kubwa kwamba utakwenda kulisimamia kwa uadilifu mkubwa ukishirikiana na wenzako waliopo pale nina uhakika mtafanya kazi kubwa hasa katika suala la uchunguzi, nataka wala rushwa wengi wafungwe hilo mimi nalitaka najua maneno kama haya hawayataki watu kuyasikia, nataka wala rushwa wengi wafungwe" alisisitiza Rais Magufuli
Aidha Rais Magufuli anasema kuwa wakifungwa wala rushwa wengi hivyo rushwa itakuwa imekwisha kwa sababu wale walaji wote watakuwa magerezani na kudai hao ndiyo wamekuwa walimu wa wala rushwa, lakini Rais aliwataka viongozi hao kutomuogopa mtu yoyote katika kutekeleza kazi yao.
"Yoyote anayehusika na rushwa huyo ni adui yangu na adui wa Watanzania wote, ni lazima ifike mahali Tanzania tuweze kuishi bila kuwa na rushwa ili manufaa haya yanayopotea kwenye rushwa yaende kwa wananchi wa kawaida, watu wanakosa madawa, wanakosa barabara, wanakosa vitu muhimu kwa sababu ya rushwa na hii ni dhambi kubwa nafikiri dini zote na mtu yoyote mwenyekupenda watu wake hawezi kutetea suala la rushwa" alisema Rais Magufuli
No comments:
Post a Comment