MADIWANI WENGINE WA CHADEMA WAJIUNGA NA CCM HAI
KAtika kile kilichoonekana hapo awali kuwa ni mkoa wa Arusha tu umekumbwa na janga la madiwani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuachia ngazi zao na wengine kuamua kujiunga na vyama vingine vya siasa nchini, leo katika HAlmashauri wa wilaya ya Hai madiwani watatu (3) wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mpinduzi (CCM).
Wakati walipokuwa wakipokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, miongoni mwa madai ya madiwani hao ni kwamba CHADEMA hakuna demokrasia kama ambavyo chama hicho kimekuwa kikijinasibu. Aidha, madiwani hao wamesema kutokana na ubabe uliomo ndani ya CHADEMA wamekuwa vipofu kiasi cha kutokuelewa namna sahihi ya kuweza kukikuza chama hicho katika zama hizi za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye anafanya mambo mengi sahihi.
Madiwani waliojiuzulu ni diwani wa Kata ya Machame Magharibi, Goodluck Kimaro, diwani wa Kata ya Weruweru na diwani wa Kata ya Mnadani, Everist Peter Kimati.
Akizungumza wakati wa kutangaza uamuzi huo, Goodluck Kimaro alisema kwamba mfano ulio wazi wa ubabe wa viongozi wa CHADEMA ni katika Halmashauri yao ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo, Freeman Mbowe alisema chama hakina uwezo wa kufanya jambo lolote dhidi ya mbunge hata kama atashindwa kutekeleza majukumu yake.
"Endapo mbunge atashindwa kutekeleza majukumu yake, chama ndio kinatakiwa kumuadhibu, lakini kwa upande wetu wa Hai hakuna Kiongozi mwenye ubavu wa kufanya hivyo. Mbunge huwa hafanyi ziara za kutembelea jimbo kama anavyotakiwa, lakini bado chama hakina sauti," alisema Goodluck Kimaro.
"Wanasema Rais amezuia mikutano ya kisiasa, hebu tuwe wakweli Rais amesema umecchaguliwa jimboni kwake kafanye mikutano kule; sasa mbona hatuwaoni wakipita huku vijini kutuhamasisha kufanya shughuli za kukikuza chama na maendeleo ya nchi?" alihoji kwa mshanga Evarist Kimati.
Aidha viongozi hao walielezea kukerwa na kauli za maudhi zinazotumiwa na viongozi wetu kuikosoa Serikali. "Hivi unaweza kumwita Rais wa nchi kuwa ni wa hovyo! Umekosa neno sahihi la kutumia. Viongozi wa juu wa Chama mbona hawawakemei wabunge wetu? Sawa, humuheshimu Rais kwa wadhifa wake basi muheshimu kama mtu aliyekuzidi umri na tumia lugha ya fursa. Tunawafundisha nini vijana wa CHADEMA? Hakika inatukera".
Hadi sasa jumla ya madiwani 9 mkoani Arusha tayari wamejiunga na CCM hivyo pamoja na hawa watatu wa Kilimanjaro inafanya idadi ya madiwani walioikimbia CHADEMA hivi karibuni kufikia 12.
MADIWANI WENGINE WA CHADEMA WAJIUNGA NA CCM HAI
Reviewed by
Unknown
on
July 27, 2017
Rating:
5
No comments:
Post a Comment