Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Monday, 7 August 2017

KOREA KASKAZINI ITATUMIA SILAHA ZAKE KWA MAREKANI NA SI NCHI NYINGINE

Korea Kaskazini haina mpango wa kutumia silaha zake za nyuklia kushambulia nchi zingine isipokuwa Marekani, Ri Hong-Yo waziri wa maswala ya kigeni wa nchi hiyo amesema.

Akizungumza mjini Manila, Ufilipino katika kongamano la mawaziri wa maswala ya kigeni kutoka muungano wa mataifa ya kusini mashariki mwa Asia (ASEAN ), Ri alisema kwamba Korea Kaskazini ni nchi inayowajibika katika matumizi ya silaha za nyuklia. "Hatuna mpango wa kutumia silaha za nyuklia kushambulia nchi yoyote, isipokuwa Marekani," alisema Ri. Ri alikashifu Marekani kwa kutilia chumvi swala la umiliki wa silaha za nyuklia na Korea Kaskazini kwa kisingizio kwamba inatishia usalama wa kimataifa.




CHANZO: China Xinhua News

No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post