Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amtaka Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kurudi wafanye mazungumzo na kumaliza tofauti zao.
“Maalim analalamika lakini malalamiko yake hayana msingi, yeye ni Katibu Mkuu anapaswa kufuata misingi ya Mwenyekiti, anatambua kuwa Mwenyekiti ni bosi kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Mwenyekiti nipo yeye aje kufanya kazi hapa."
"Maalim ni mkongwe wa siasa tunataka kuwa na maelewano, nampigia simu hapokei, nasikia sasa hivi akija Dar es Salaam anakwenda uchochoroni huko Magomeni wakati tuna ofisi hapa nzuri, Katibu Mkuu unauzoefu wa kisiasa tufanye majadiliano ofisi zetu ziko hapa njoo tuzungumze,” alisisitiza Lipumba
No comments:
Post a Comment