Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Wednesday, 9 August 2017

WATU WAWILI WALIPIGWA RISASI NA KUFA LEO KATIKA MAKAZI DUNI YA MATHARE MJINI NAIROBI

Watu wawili walipigwa risasi na kufa na wengine kadhaa walijeruhiwa katika makazi duni ya Mathare mjini Nairobi hivi leo (Jumatano) katika machafuko ya uchaguzi nchini Kenya.
 
Hata hivyo, afisa wa polisi wa Nairobi  ambaye hakutaka kujulikani alisema hawa wawili walipigwa risasi baada ya kujaribu kushambulia maofisa wa polisi wakitumia panga katika makazi duni ya Mathare.
 
Mamia ya vijana huko Kisumu,  Homa bay  katika magharibi mwa Kenya na Mathare jijini Nairobi walifanya maandamano ya amani baada ya kutagaswa kuwa rais Uhuru Kenyatta alikuwa aliendelea kuongoza Raila Odinga.
 
Odinga alikataa matokeo ya urais, akisema kuwa mitambo ya  tume ya uchaguzi  ilikuwa imeingiliwa na wadukuzi na kuwapatia nafasi ya kuimbiwa kwa kura.

No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post