Wakati Victor Mlotshwa alipokataa, wakulima hao walimtishia kuwa watamweka ndani ya jeneza hilo pamoja na nyoka.
Washtakiwa hao Willem Oosthuizen na Theo Jackson, walikamatwa mwezi Novemba mwaka jana, baada ya video ya kitendo hicho kilipowekwa mitandaoni.
Walisema kuwa, Bwana Mlotshwa alipitia kwenye shamba lao liliko katika jimbo la Mpumalanga, bila ya kuwa na idhini, na walikuwa wakimuadhibu.
Katika kusikizwa kwa kesi hiyo awali, jaji wa mahakama alisema kuwa wakulima hao walikuwa wakatili na waliojaa tabia za ubaguzi wa rangi.
No comments:
Post a Comment