Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Thursday, 10 August 2017

MWANARIADHA SIMBU ASEMA MEDALI ALIYOIPATA NI ZAWADI KWA WATANZANIA

Mwanariadha Mtanzania, Alphonce Felix Simbu, wiki iliyopita alifanikiwa kushinda medali ya
shaba katika mashindano ya Mbio za Dunia kwa upande wa Marathoni zinazoendelea London, England na kusema kuwa medali hiyo ni zawadi kwa watanzania.

Simbu mwaka jana katika mashindano ya Olimpiki jijini Rio De Janeiro, Brazili alishika nafasi ya tano, kabla ya Januari mwaka huu kushinda medali ya dhahabu katika mbio za Standard Chartered Marathon zilizofanyika India kwa kushika nafasi ya kwanza baada
ya kutumia saa 2:09: 32.

Mwanariadha huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa iliyoshiriki mashindano hayo ikiwa na wawakilishi nane, amefanikiwa kushinda medali
hiyo baada ya miaka 12.

Simbu ameshinda medali kwa kushika nafasi ya tatu baada ya kutumia muda wa saa 2:09:51, akiwa nyuma ya mshindi wa kwanza, Mkenya Geofrey Kirui aliyetumia muda wa saa  2:08:27, huku mshindi wa pili ni Muethiopia Tamirat Tola akitumia muda wa saa 2:09:47.


No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post