Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya (IEBC) hatimaye imemtangaza Uhuru Kenyatta kama mshindi wa uchaguzi wa urais wa Agosti 8.
Mwenyekiti wa tume hiyo Bw Wafula Chebukati ametangaza rasmi matokeo hayo katika ukumbi wa Bomas, jijini Nairobi karibu saa nne unusu usiku huu wa leo baada ya tangazo hilo kusubiriwa kuanzia saa sita mchana.
Rais Kenyatta ataapishwa upya kuendelea kuhudumu muhula wake wa pili hadi mwaka wa 2022 uchaguzi mwingine utakapofanywa. #Decision2017
No comments:
Post a Comment