Serikali ya Tanzania imekanusha kuingilia masuala ya kwamba imekuwa ikiingilia uchaguzi wa Kenya unaotarajia kufanyika agosti nane.
Tuhuma hizo za kuingilia uchaguzi nchini Kenya zimekanushwa leo jumatatu jijini Dar es Salaam na Waziri wa wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga.
"Hatujawahi kuingiliana, Kenya haijawahi kuingilia Tanzania na Tanzania haijawahi kuingilia Kenya, leo kwa nini iwe hivyo?"
Akizungumza na waandishi wa habari leo jiji Dar es Salaam, Waziri Mahiga katika mkutano na waandishi, alikuwa na lengo la kuzungumzia pia vikwazo vya kibiashara baina ya Tanzania na Kenya vilivyoibuka hivi karibuni.
"Sisi tunautaratibu wetu wa Afrika Mashariki tunatembeleana, na tunafanya kazi pamoja," amesema.
Mahiga amesema hawa wanaosambaza taarifa hizi kwenye vyombo vya habari au ambao wanazungumza bungeni wanalo lao jambo.
"Tuwe macho inawezekana hata watu wa nje wanaingilia kujaribu kutugombanisha...
lakini nachukua nafasi hii tena kwa niaba ya serikali na rais wangu kuwahakikishia watu wa Kenya, serikali ya Kenya, vyombo vya habari hatuingilii uchaguzi wa Kenya alissema.
Aldi shoppers clear shelves of bargain £3.49 Christmas tipple despite
imposing a limit on customers
-
SHOPPERS have flocked to Aldi to get their hands on a festive tipple so
good, it has a limit.
The viral Cairanne Wine is back on shelves in Aldi, with t...
11 minutes ago
No comments:
Post a Comment