MATOKEO YA UCHAGUZI KENYA: Rais mteule wa Kenya UHURU KENYATTA awashukuru wakenya na Tume huru ya uchaguzi.
Awapongeza walioshinda na walioshindwa, pamoja na waangalizi wa uchaguzi.
Awataka walioshindwa kutokuwa maadui kwani wote wanalengo moja la kujenga taifa la Kenya.
Amtaka Raila Odinga, kushirikiana na Jubilee na kwamba wako tayari kwa majadiliano kwaajili ya kuijenga KENYA pamoja.
Ameomba amani na kuwataka WAKENYA kuepuka machafuko kwani wao ni ndugu na kwamba wao wanasiasa wataondoka na kuiacha Kenya.
No comments:
Post a Comment