Serikali imekitaifisha kiwanda cha kusindikiza ngozi cha Mwanza Tanneries kilichopo eneo la viwanda Ilemela mkoani Mwanza, baada ya wamiliki wake kushindwa kukiendeleza kuanzia mwaka 1998 hadi sasa, huku ikibaini kuwepo kwa udanganyifu wa umiliki wa kiwanda hicho uliodaiwa kufanywa na kampuni ya Quality group.
Uamuzi huo umetangazwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza john Mongella mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo, wakiwemo pia wawakilishi wa kampuni ya Caspian na Quality group zilizoshindwa kutekeleza masharti ya mkataba wa kukiendeleza kiwanda hicho.
CHANZO: ITV
No comments:
Post a Comment