Rais John Magufuli amekataa ombi la kukisamehe kodi la kiwanda cha saruji cha Kilimanjaro kilichopo jijini Tanga kwa maelezo kuwa ni kinyume na sheria.
Rais Magufuli ametoa msimamo huo wakati akitoa hotuba yake katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kiwanda hicho na kutumia fursa hiyo kujibu maombi yaliyokuwa katika risala ya kiwanda hicho, ambacho kilitaka kisamehewe kodi kwa muda wa miaka 10 kutokana na deni kubwa ambalo kinadaiwa katika taasisi za kifedha, zilizokopwa kama mtaji wa kukianzisha.
Sababu nyingine za kutaka kiwanda hicho kisamehewe kodi ni kutokana na mchango wake katika shughuli za kijamii ikiwemo kuchangia madawati na vyumba vya madarasa katika shule za jiji hilo pamoja na kusaidia huduma za maji.
Katika majibu yake, rais Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake inahimiza viwanda ili iweze kupata mapato kupitia kodi, kwahiyo haiwezi kufanya uamuzi wa kusamehe kodi na kujikosesha mapato.
Kiwanda hicho ambacho tayari kilikwishaanza uzalishaji, kina malengo ya kuongeza uzalisha kutoka tani 300 hadi tani 3000 za saruji.
No comments:
Post a Comment