Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Wednesday, 9 August 2017

Manji arudi mahakamani tena leo

Mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji leo pia kazikamata headlines za hard news baada ya kurudi tena Mahakamani.

Katika kurudi kwake Mahakamani leo Serikali iliomba Manji akahojiwe na Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA kuhusu masuala ya kodi lakini maombi hayo yalitupiliwa mbali na Mahakama.

Maombi ya kutaka Manji ahojiwe na TRA, yamewasilishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa ambaye amedai wanaiomba Mahakamani itoe kibali ili Manji ahojiwe kisha atarudisha ndani ya muda wa kazi kabla haujaisha.

No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post