Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Saturday, 26 August 2017

Alikiba awapagawisha

Msanii Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' ambao ameuachia jana amevunja rekodi na kuwapagawisha mashabiki katika mtandao wake wa YouTube katika account yake ya 'Vevo' kutokana na wimbo huo kuwa na kasi kubwa ya watazamaji.

Msanii Alikiba


Katika mtandao huo ambao Alikiba ameweza kuweka jumla ya video mbili 'Aje Remix' ambayo kwa zaidi ya miezi sita imeweza kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja na kuchangiwa kwa jumla ya 'comment' 1000 huku video yake mpya 'Seducce me' ndani ya masaa 24 imeweza kufikisha watazamaji zaidi ya laki sita na kuchagiwa na watu zaidi ya elfu 6000 ndani ya muda mfupi.  

Kasi hii si ya kawaida ukilinganisha na video ambayo ipo toka miezi sita iliyopita lakini ni wazi kuwa huenda kasi hii kubwa ya utazamwaji wa video hii unachangiwa na mapokeo mazuri ya washabiki wa muziki wa Alikiba ambao wanajikuta kila wakati wakitaka kuitazama video hiyo.

Haya ni baadhi ya maoni ya watu ambao wameweza kuitazama video hiyo na kufunguka ya moyoni mwao 

Friday, 25 August 2017

Sikujua alichokifanya - Fid Q

Rapa Fid Q amefunguka na kuonyesha hisia zake juu ya mambo mbalimbali ambayo yametokea baada ya moja ya msanii wa bongo kufanya 'Remix' ya wimbo wake 'Fresh' na kusema yeye mwenyewe alikuwa hajui kama msanii huyo alimchana hasimu wake Alikiba.

Fid Q amedai kuwa yeye si mfuatiliaji wa muziki wa bongo fleva hivyo kuna mambo mengi kuwahusu wasanii hao hayajui na kudai hata aliposikia kwenye 'Remix' hiyo neno Cinderela alijua kuwa amemaanisha ni mwanamke na kudai hakufikiri wala kuwaza kama lilikuwa ni dongo kwa Alikiba. 

"Aliposema ule mstari sijui msinifananishe na Cinderela mimi nilichukulia ile Cinderela kama usinifananishe na mtoto wa kike, niwakumbushe mimi ni mtu wa hip hop sijui chochote kile kuhusu bongo fleva, najua majina ya wasanii wa bongo fleva ila sijui chochote kuhusu miziki yao, hivyo kile alichoimba ni hisia zake yeye kwa hiyo niseme tu mimi mwenyewe nilifichiwa 'white' sikujua ile Cinderela iliyoimbwa mle ni wimbo wa Alikiba na sikujua kama ni dongo kwa Alikibaalisema Fid Q 

Aidha Fid Q amedai kutokana na kile alichofanya Ommy Dimpoz kupitia mtandao wake wa Instgram kujibu ile ngoma kimemuondolea vibe kabisaa na kudai saizi hata ukimuuliza 'Fresh' yeye atakwambia siyo 'Fresh', mbali na hilo Fid Q amesema ndoto yake sasa ni kuona anakuja kuwakutanisha wasanii hao wawili ili waweze kumaliza hizo tofauti zao kwa sababu yeye wote yuko nao sawa na hana tatizo nao. 

MGUFULI ZIARANI KIGAMBONI LEO

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana pamoja na kuzungumza na abiria mbalimbali wakati akisubiri kuvuka kwa kutumia usafiri wa Pantoni kuelekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam 25 Agosti 2017.
Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda kufanyia kazi ombi la wananchi wa eneo hilo la kutaka kujengewa kituo cha Daladala.
Picha/Ikulu, Tanzania





MAKONDA: BAADHI YA ASKARI WANASHIRIKI KATIKA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema amebaini baadhi ya askari polisi Jijini Dar es salaam wanashiriki biashara ya dawa za kulevya na wengine wanashiriki kuvusha kobe wanaopelekwa nje ya nchi.

 Makonda ameyasema hayo Jijini Dar es salaam baada ya kupokea pikipiki 10 kutoka kwa wadau wa maendeleo.

Makonda amelitaka jeshi la polisi kuhakikisha askari hao waliokiuka maadili ya kazi yao watafunguliwa mashtaka.


Thursday, 24 August 2017

"Nataka wala rushwa wengi wafungwe" - Magufuli

Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kusema anataka watu wanaokula rushwa wengi wao wafungwe kwani watu hao wanasababisha watu wakose barabara, madawa na kukosa maendeleo kutokana na watu kula rushwa.
Rais John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akimuapisha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali, John Julius Mbungo leo Ikulu jijini Dar es Salaam na kumtaka afanye kazi kuhakikisha rushwa inakomeshwa. 
"Umepewa hilo jukumu kalisimamie na tunaimani kubwa kwamba utakwenda kulisimamia kwa uadilifu mkubwa ukishirikiana na wenzako waliopo pale nina uhakika mtafanya kazi kubwa hasa katika suala la uchunguzi, nataka wala rushwa wengi wafungwe hilo mimi nalitaka najua maneno kama haya hawayataki watu kuyasikia, nataka wala rushwa wengi wafungwe" alisisitiza Rais Magufuli 
Aidha Rais Magufuli anasema kuwa wakifungwa wala rushwa wengi hivyo rushwa itakuwa imekwisha kwa sababu wale walaji wote watakuwa magerezani na kudai hao ndiyo wamekuwa walimu wa wala rushwa, lakini Rais aliwataka viongozi hao kutomuogopa mtu yoyote katika kutekeleza kazi yao.
"Yoyote anayehusika na rushwa huyo ni adui yangu na adui wa Watanzania wote, ni lazima ifike mahali Tanzania tuweze kuishi bila kuwa na rushwa ili manufaa haya yanayopotea kwenye rushwa yaende kwa wananchi wa kawaida, watu wanakosa madawa, wanakosa barabara, wanakosa vitu muhimu kwa sababu ya rushwa na hii ni dhambi kubwa nafikiri dini zote na mtu yoyote mwenyekupenda watu wake hawezi kutetea suala la rushwa" alisema Rais Magufuli  


Dr. SLAA: KAMPUNI INAYOSHIKILIA BOMBARDIER ILIKWISHATUHUMIWA KWA UZEMBE BUNGENI

Aliyekuwa Mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, ameibuka na kudai kwamba kampuni ya ujenzi inayotajwa kuishikilia ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-Dash 8, ilikwishatuhumiwa kwa uzembe bungeni.

Kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd, ndiyo, kwa mujibu wa maelezo ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, imeishikilia ndege hiyo iliyonunuliwa na Tanzania nchini Canada. Uamuzi huo wa kuishikilia unatajwa kuwa ni utekelezaji wa matakwa ya Mahakam a ya Kimataifa ya Usuluhishi, kuiwezesha  kampuni hiyo kulipwa deni lake la dhidi ya serikali ya Tanzania la dola za Marekani milioni 38.7 ambazo ni takriban shilingi bilioni 87.

Msingi wa deni hilo ni kuvunjwa kwa mkataba wa kati ya serikali na kampuni hiyo wa ujenzi wa barabara kutoka eneo la Wazo Hill jijini Dar es Salaam hadi Bagamoyo, mkoani Pwani.

Akizungumzia kadhia hiyo Dk. Slaa alisema pamoja na hali hiyo, kampuni  ya ujenzi ya Stirling si “nadhifu” katika kazi zake na hata wabunge walikwishailalamikia bungeni mwaka 2005, akisisitiza kuwa, yeye ni kati ya wabunge waliopata kuilalamikia kampuni hiyo.

Katika mawasiliano yake na gazeti hili, Dk. Slaa aliyepata kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 alisema; “Siamini kama serikali huwa inavunja mikataba ovyo. Kauli hiyo ni vema ikathibitishwa kwa ushahidi na hasa kuonyesha ni vipengele vipi vya mkataba vimevunjwa au sheria ipi imekiukwa. Si vema kutoa kauli za jumla jumla bila uthibitisho.

Kauli hiyo ya Slaa inapingana na madai ya Lissu ya hivi karibuni kwamba mkataba kati ya serikali na kampuni hiyo ulivunjwa ovyo, kinyume cha utaratibu na ndio maana, kampuni hiyo imekwenda kushitaki katika Mahakama ya Kimataifa na kushinda kesi.

Slaa anaeleza zaidi; “Kama ni suala la kushikiliwa Bombardier ninachokumbuka ni kuwa kampuni husika ilishindwa kumaliza ujenzi wa barabara hiyo (Wazo Hill hadi Bagamoyo) katika muda uliotajwa  ndani ya mkataba.”

Alieleza kwamba hata sehemu ambayo kampuni hiyo ilikamilisha kipande cha ujenzi wa barabara, basi, ujenzi huo ulikuwa chini ya kiwango na pale kampuni hiyo ilipopewa muda kurekebisha udhaifu huo ilishindwa kufanya hivyo.

“Bungeni tulipiga sana kelele kuhusu ucheleweshaji huo na kazi isiyoridhisha. Nilikuwa Mbunge wa Karatu wakati huo na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na kumbukumbu ziko kwenye hansard, tatizo watu hawapendi kufanya utafiti,” alisema Slaa.

Akizungumzia suala la Tanzania kushindwa kesi kwenye Mahakama ya Kimataifa, Dk. Slaa alisema; “..hiyo haina maana ya kuwa kampuni hiyo ilikuwa “absolutely” na haki. Mahakama zinategemea zimeelekea wapi hasa hizi za biashara ya kimataifa ambazo kimsingi zinalinda maslahi ya nchi zao. Hili nililizungumzia sana bungeni hasa kutokana na uzoefu wangu katika Bunge la ACP/EU – Joint Assembly ambalo nilikuwa nikiwalisha Bunge la Tanzania mwaka 1996 hadi 2000 .Tuliitaka serikali yetu ichukue hatua bahati mbaya haikuchukua hatua.”

NANI KUCHEZA NA NANI ULAYA?

Nani kucheza na nani Ulaya? Droo ya Klabu Bingwa Ulaya 2017-18

Uingereza inawakilishwa na timu sita msimu huu. Chelsea, Tottenham, Manchester City, Liverpool, Manchester United na Celtic.

Timu hizo zitafahamu zitakutana na nani katika droo itakayofanyika Monaco leo saa moja usiku saa za Afrika Mashariki.

Droo itakuwa ya timu 32 na itatoa makundi manane.

Real Madrid walishinda Klabu Bingwa Ulaya mwezi Juni mwaka huu mjini Cardiff, na kuwa timu ya kwanza kushinda kombe hilo – katika enzi za Klabu Bingwa- mara mbili mfululizo.

Kuna ‘vyungu’ vinne vyenye timu nane, huku kila timu moja katika chungu ikiunda kundi lake, ingawa timu kutoka chama kimoja cha soka haziwezi kupangwa katika kundi moja.

Mabingwa wa England, Chelsea watakuwa katika ‘chungu’ namba moja, pamoja na Real Madrid, Bayern Munich, Juventus, Benfica, Shakhtar Denotsk, Monaco na Spartak Moscow.

Chelsea, mabingwa wa Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2012, wanarejea katika michuano hii baada ya kukosekana kwa msimu mmoja na wamerejea baada ya kushinda EPL chini ya Antonio Conte.

Manchester United nao wameingia baada ya kushinda Ligi ya Europa, chini ya Jose Mourinho, ambaye alishinda Klabu Bingwa Ulaya na Porto mwaka 2004 na mwaka 2010 akiwa na Inter Milan.

Manchester United walioondolewa kwenye michuano hii katika ngazi ya makundi msimu wa 2015-16, wapo katika ‘chungu’ cha pili, pamoja na Manchester City, Barcelona, Atletico Madrid, Paris Saint –Germain, Borussia Dortmund, Sevilla na FC Porto.

Tottenham na Liverpool watakuwa katika ‘chungu’ namba tatu, pamoja na Napoli, Basel, Olympiakos, Anderlecht, Roma, na Besitkas.

Celtic watakuwa ‘chungu’ namba nne pamoja na CSKA Moscow, Qarabag, Sporting CP, APOEL, Feyenoord, Maribor, na RB Leipzig.

Mechi za makundi zitaanza Septemba 12 na 13.
Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya itachezwa kwenye dimba la NSK Olimpiyskyi mjini Kiev, Mei 26, 2018.

Droo ya Ligi ya Europa itafanyika Monaco siku ya Ijumaa.

Everton, wanaocheza usiku huu watakuwa na matumaini ya kuungana na Arsenal, ambao hawachezi Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.

Diamond akamatwa kwa kusababisha ajali

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia dereva wa basi lenye namba za usajili T 438 ADR Charles Diamond, kwa kusababisha ajali iliyopoteza uhai wa watu mkoani Morogoro na kusababisha majeraha kwa baadhi ya watu.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Ulrich Matei


Akitoa taarifa ya ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Kamanda wa Polisi mkoani humo Urlich Matei, amesema mpaka sasa idadi kamili ya watu waliofariki kutokana na ajali hiyo ni watu watatu, ambapo wawili ni wanawake na mmoja ni mwanaume, huku mmoja wao akiwa ni mwanafunzi.

Majeruhi wa ajali hiyo ni 27 ambao wamepelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, lakini suala la utambuzi wa miili ya marehemu bado halijafanyika mpaka pale uchunguzi utakapofanyika.

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi iliyohusisha gari aina ya daladala ikielekea Mvumi kugonga treni iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, kulikopelekea kuburuzwa kwa gari hiyo na kusababisha vifo.

Monday, 21 August 2017

Roma aikana CHADEMA

Msanii Roma Mkatoliki ambaye anaimba muziki wa Hip hop kwenye game ya bongo, amekikana chama cha CHADEMA na kusema kuwa hajawahi kuwa mwanachama wa chama hicho kama ambavyo wengi wanaamini, na hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote.

Roma ambaye hivi karibuni alikutwa na sakata la kutekwa na kuibua sintofahamu nyingi, amesema kwamba hajawahi kuwa mwanasiana na hajawahi kuwa na kadi ya chama chochote.

"Mtu akisema nipo kwenye siasa za upinzani siyo jambo sahihi na siyo jambo ambalo nalifurahia kwa sababu mimi sina kadi ya chama chochote, mimi siyo mwanachama wa chama chochote, na mtu akisema nusu ya watanzania wanajua uko CHADEMA sijui ana uthibitisho gani kwa sababu sina kadi ya chama, na mimi nasimama kati kati", alisema Roma Mkatoliki.

Roma hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya wa 'Zimbabwe' ambao umeibua hisia kwa wengii, kwa kuelezea tukio zima la utekwaji wake ulivyokuwa. Wimbo ambao mpaka sasa umeweza kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja na kitu ndani ya wiki moja. 

MCHEZO WA KWANZA PSG: Baada ya kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 198,

 Baada ya kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 198, kutoka Barcelona na kuhamia kwa miamba ya soka ya Ufaransa Paris Saint-Germain, mbrazil Neymar Junior afanya kile kilichotarajiwa na wengi kwenye mechi yake ya nyumbani dhidi ya timu ya Toulouse iliyochezwa kwenye uwanja wa Parc des Princes.

Hadi mwisho wa mchezo miamba hiyo ya soka nchini Ufaransa iliibuka na ushindi wa mabao 6 -2



HABARI YA ASUBUHI LEO JUMATATU 21.08.2017 TUMEKUWEKEA VICHWA VYA MAGAZETI YOTE YA LEO HAPA

























Sunday, 20 August 2017

Magufuli kuingilia ugomvi wa Kanisa!?

Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Temeke limemuomba Rais Dkt John Pombe Magufuli kuingilia kumaliza mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 unaohusu umiliki wa kiwanja kilichopo Kitalu D Mtaa wa Everest jirani na Hospitali ya wilaya ya Temeke.

Mdhamini wa Kanisa la EAGT nchini Mchungaji Christom Isack Ngowi ametoa kauli hiyo kufuatia notisi inayowataka kuhamisha mali zote za kanisa kabla ya kesho Agosti 21, siku ambayo Manispaa ya Temeke imepanga kubomoa eneo hilo, kitendo ambacho waumini na viongozi wa kanisa hilo wamesema kingesubiri maamuzi ya barua waliyomuandikia Rais Magufuli kuhusu mgogoro huo.

Katika maelezo yao, viongozi na waumini wa kanisa hilo wameshangazwa na kile walichoeleza kuwa ni kutotekelezwa kwa maagizo ya mawaziri wa zamani wa ardhi akiwemo marehemu Mustafa Nyang'anyi na mwenzake Marcel Bujiku Komanya, ambao katika nyakati tofauti walizitaka mamlaka kulipatia kanisa la EAGT Temeke umiliki wa eneo hilo.

Kiwanja hicho kinagombewa kati yao na mfanyabiashara mmoja wa eneo hilo.

CHANZO: EATV

Maelfu ya watu waliandamana mjini Boston, Marekani, kupinga ubaguzi na chuki

Maelfu ya watu waliandamana mjini Boston, Marekani, kupinga ubaguzi na chuki, ikiwa ni wiki moja, baada ya maandamano ya Wanazi mamboleo na wanaotukuza
utukufu wa watu weupe mbele ya binadamu wengine, yaliyofanyika katika mji wa Charlottesville, Virginia, kugeuka kuwa vurugu.
Kamishina wa Polisi katika mji huo, Willian Evans, amesema watu 27 wamekamatwa na baadhi ya maafisa wa jeshi hilo walirushiwa chupa zilizojazwa mkojo.
Hata hivyo, amesema licha ya kasoro hizo maandamano hayo yalikuwa ya amani na amefurahishwa na jinsi watu walivyojitokeza na kupinga ubaguzi.
(Picha:CNN)

WANACHAMA 1,217 WAPITISHA MABADILIKO KATIKA KLABU YA SIMBA, MMOJA TU APINGA

Dar es Salaam. Wanachama wa Simba wamepitisha mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo kwenye mkutano mkuu maalumu uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Jumapili.

Wanachama hao wamebariki mabadiliko hayo baada ya kupiga kura za kukubali au kukataa ambapo ni mwanachama mmoja kati ya ya 1,217 alipinga.

Katika mkutano huo uliofanyija jijini Dar es Salaam leo Jumapili, wanachama hao walipiga kura ya wazi wakihojiwa na Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah.

WANACHAMA SIMBA SC KUANZA NA ASILIMIA 10 ZA HISA ZA KLABU

"Wanachama Simba kuanza na asilimia 10 hisa za klabu"

Imani Makongoro

Dar es Salaam. Mkutano Mkuu wa Mabadiliko ya Uendeshaji ya Klabu umefafanua kwamba bilioni 40 ndiyo mtaji wa hisa kuelekea kwenye mabadiliko ya uendeshaji wa klabu lakini ukasisitiza katika mabadiliko hayo wanachama wataanza na asilimia 10.

Taarifa ya mkutano huo imefafanua kwamba, mabadiliko ya uendesha wa klabu yataanza na mtaji wa bilioni 40.

"Katika mtaji huo, wanachama watakuwa na asilimia 50, lakini kwa kuanzia itaanza na asilimia 10 (sawa na bilioni 4) na asilimia nyingine 40 itatafuta wawekezaji wa kuwasaidia kukuza mtaji na wanachama kuendelea kurudisha taratibu.

"Ieleweke, wanachama watakuwa na asilimia 50, lakini wataanza na asilimia 10 sababu uwezo wa kuweka mtaji wa asilimia 50 kwa mara moja haupo.

"Asilimia nyingine 50 iliyosalia klabu itawakaribisha wawekezaji ambao lazima wawe na bilioni 20," ilieleza taarifa ya klabu hiyo ambayo imetolewa kwenye mkutano unaoendelea leo Jumapili jijini Dar es Salaam

ZITO KABWE:Suala la Ndege yetu kuzuiwa Canada lisifanywe ni ushabiki

Suala la Ndege yetu kuzuiwa Canada lisifanywe Ni suala la ushabiki Kama ushabiki wa mpira. Ni suala la Nchi hili na mjadala wake uwe na hadhi hiyo.
Kitendo cha Msemaji wa Serikali kulaumu wanasiasa Kwa jambo la kisheria Kama hili ni utoto. Hakuna mwanasiasa anayeweza kushirikiana na kampuni za kigeni kuhujumu nchi. Mimi binafsi filosofia yangu ni rahisi Sana ' My Country, Right or Wrong '. Maneno yanayosambazwa kuwa nimeshiriki kuwezesha Ndege ya Bombardier iliyonunuliwa na Serikali Kwa niaba ya ATCL kukamatwa huko Canada ni takataka tu zinazosambazwa na wapika propaganda.
Serikali lazima ifahamu kuwa ni lazima ihojiwe na iwe tayari kutoa majibu. Sisi kama vyama vilivyo Nje ya Serikali Ni wajibu wetu kuhoji jambo lolote. Pia ni haki yetu kupata Taarifa zozote kutoka mahala popote zitakazosaidia kuisimamia Serikali. Wajibu wa Serikali ni kujibu hoja zinazoibuliwa. Majibu ya Msemaji wa Serikali yanataka kuligeuza suala hili kuwa la kisiasa na watu wameangukia kwenye ushabiki huo. Hili ni suala la kisheria na suala la nchi ambayo sisi wote tuna maslahi ya kuona inakwenda mbele.
Nchi kudaiwa sio dhambi. Hata mataifa makubwa duniani yanadaiwa. Watu binafsi tunadaiwa sembuse Serikali? Mimi ninadaiwa madeni ya uchaguzi mpaka Sasa na wengine wamenipeleka mahakamani. Sio dhambi kudaiwa. Muhimu ni 1) Deni limetokana na Nini? Ni maamuzi mabovu ya kisiasa? 2) unalipa deni hilo au kuweka mikakati ya kulipa?
Serikali yetu inafahamu kuwa nchi yetu Ina madeni mengi na miongoni Mwa madeni hayo yameshaamuliwa na Mahakama. Kinachopaswa ni kuwa na MAARIFA ya kupita ili kuzuia Mali zetu nje kuzuiwa Kama ilivyo Kwa Ndege Hii. Serikali iwe wazi kuhusu suala hili la Ndege. Je ile ya Boeing ( Terrible Teen ) ipo salama? Madeni mengine yenye amri ya mahakama ni yepi? Kwanini Serikali inasubiri kuhojiwa Ndio itoe Taarifa?
Hii ni nchi yetu sote. Hakuna mwenye hatimiliki ya ukweli. Ukweli pia haupendi kupindwa pindwa. Serikali itoke kueleza nini kimetokea mpaka Ndege kuzuiwa, iachane na tabia ya hovyo ya kutafuta mchawi ' kwamba eti wanasiasa Ndio wamesababisha '. Kutafuta mchawi ni kutowajibika Kwa maamuzi ya Serikali yenyewe.
Aliandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wa Facebook.

Haya Hapa ni maoni ya baadhi ya wachangiaji wa mjadala huo wa Mh. Zitto Kabwe







Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post