Latest News

Comments

Featured
Featured

Gallery

Technology

Video

Games

Recent Posts

tanganyikanews.com

tanganyika we speak the truth always

Saturday, 26 August 2017

Alikiba awapagawisha

Msanii Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' ambao ameuachia jana amevunja rekodi na kuwapagawisha mashabiki katika mtandao wake wa YouTube katika account yake ya 'Vevo' kutokana na wimbo huo kuwa na kasi kubwa ya watazamaji.

Msanii Alikiba


Katika mtandao huo ambao Alikiba ameweza kuweka jumla ya video mbili 'Aje Remix' ambayo kwa zaidi ya miezi sita imeweza kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja na kuchangiwa kwa jumla ya 'comment' 1000 huku video yake mpya 'Seducce me' ndani ya masaa 24 imeweza kufikisha watazamaji zaidi ya laki sita na kuchagiwa na watu zaidi ya elfu 6000 ndani ya muda mfupi.  

Kasi hii si ya kawaida ukilinganisha na video ambayo ipo toka miezi sita iliyopita lakini ni wazi kuwa huenda kasi hii kubwa ya utazamwaji wa video hii unachangiwa na mapokeo mazuri ya washabiki wa muziki wa Alikiba ambao wanajikuta kila wakati wakitaka kuitazama video hiyo.

Haya ni baadhi ya maoni ya watu ambao wameweza kuitazama video hiyo na kufunguka ya moyoni mwao 

Friday, 25 August 2017

Sikujua alichokifanya - Fid Q

Rapa Fid Q amefunguka na kuonyesha hisia zake juu ya mambo mbalimbali ambayo yametokea baada ya moja ya msanii wa bongo kufanya 'Remix' ya wimbo wake 'Fresh' na kusema yeye mwenyewe alikuwa hajui kama msanii huyo alimchana hasimu wake Alikiba.

Fid Q amedai kuwa yeye si mfuatiliaji wa muziki wa bongo fleva hivyo kuna mambo mengi kuwahusu wasanii hao hayajui na kudai hata aliposikia kwenye 'Remix' hiyo neno Cinderela alijua kuwa amemaanisha ni mwanamke na kudai hakufikiri wala kuwaza kama lilikuwa ni dongo kwa Alikiba. 

"Aliposema ule mstari sijui msinifananishe na Cinderela mimi nilichukulia ile Cinderela kama usinifananishe na mtoto wa kike, niwakumbushe mimi ni mtu wa hip hop sijui chochote kile kuhusu bongo fleva, najua majina ya wasanii wa bongo fleva ila sijui chochote kuhusu miziki yao, hivyo kile alichoimba ni hisia zake yeye kwa hiyo niseme tu mimi mwenyewe nilifichiwa 'white' sikujua ile Cinderela iliyoimbwa mle ni wimbo wa Alikiba na sikujua kama ni dongo kwa Alikibaalisema Fid Q 

Aidha Fid Q amedai kutokana na kile alichofanya Ommy Dimpoz kupitia mtandao wake wa Instgram kujibu ile ngoma kimemuondolea vibe kabisaa na kudai saizi hata ukimuuliza 'Fresh' yeye atakwambia siyo 'Fresh', mbali na hilo Fid Q amesema ndoto yake sasa ni kuona anakuja kuwakutanisha wasanii hao wawili ili waweze kumaliza hizo tofauti zao kwa sababu yeye wote yuko nao sawa na hana tatizo nao. 

MGUFULI ZIARANI KIGAMBONI LEO

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana pamoja na kuzungumza na abiria mbalimbali wakati akisubiri kuvuka kwa kutumia usafiri wa Pantoni kuelekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam 25 Agosti 2017.
Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda kufanyia kazi ombi la wananchi wa eneo hilo la kutaka kujengewa kituo cha Daladala.
Picha/Ikulu, Tanzania





MAKONDA: BAADHI YA ASKARI WANASHIRIKI KATIKA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema amebaini baadhi ya askari polisi Jijini Dar es salaam wanashiriki biashara ya dawa za kulevya na wengine wanashiriki kuvusha kobe wanaopelekwa nje ya nchi.

 Makonda ameyasema hayo Jijini Dar es salaam baada ya kupokea pikipiki 10 kutoka kwa wadau wa maendeleo.

Makonda amelitaka jeshi la polisi kuhakikisha askari hao waliokiuka maadili ya kazi yao watafunguliwa mashtaka.


Thursday, 24 August 2017

"Nataka wala rushwa wengi wafungwe" - Magufuli

Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kusema anataka watu wanaokula rushwa wengi wao wafungwe kwani watu hao wanasababisha watu wakose barabara, madawa na kukosa maendeleo kutokana na watu kula rushwa.
Rais John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akimuapisha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali, John Julius Mbungo leo Ikulu jijini Dar es Salaam na kumtaka afanye kazi kuhakikisha rushwa inakomeshwa. 
"Umepewa hilo jukumu kalisimamie na tunaimani kubwa kwamba utakwenda kulisimamia kwa uadilifu mkubwa ukishirikiana na wenzako waliopo pale nina uhakika mtafanya kazi kubwa hasa katika suala la uchunguzi, nataka wala rushwa wengi wafungwe hilo mimi nalitaka najua maneno kama haya hawayataki watu kuyasikia, nataka wala rushwa wengi wafungwe" alisisitiza Rais Magufuli 
Aidha Rais Magufuli anasema kuwa wakifungwa wala rushwa wengi hivyo rushwa itakuwa imekwisha kwa sababu wale walaji wote watakuwa magerezani na kudai hao ndiyo wamekuwa walimu wa wala rushwa, lakini Rais aliwataka viongozi hao kutomuogopa mtu yoyote katika kutekeleza kazi yao.
"Yoyote anayehusika na rushwa huyo ni adui yangu na adui wa Watanzania wote, ni lazima ifike mahali Tanzania tuweze kuishi bila kuwa na rushwa ili manufaa haya yanayopotea kwenye rushwa yaende kwa wananchi wa kawaida, watu wanakosa madawa, wanakosa barabara, wanakosa vitu muhimu kwa sababu ya rushwa na hii ni dhambi kubwa nafikiri dini zote na mtu yoyote mwenyekupenda watu wake hawezi kutetea suala la rushwa" alisema Rais Magufuli  


Videos

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post