UINGEREZA: Mwanamke, Arafa Nassib mwenye umri wa miaka 48 amehukumiwa kwenda jera kutumikia kifungo cha miaka miwili na miezi sita kwa kosa la kudanganya kuwa amefariki ambapo cheti chake cha kifo kinaonyesha alifia visiwani Zanzibar.
Mwanamke huyo alimuelekeza mwanae wa kiume kuzitaka Mamlaka kumpatia Bima yenye thamani ya zaidi ya milioni 398.
Mahakama imebaini kuwa mwanamke huyo alikuwa akidaiwa mkopo wa thamani ya zaidi ya milioni 234 ndipo aliposafiri kwenda Zanzibar na taarifa kutoka zikidai amefariki katika ajari ya gari.
makachero walipofuatilia lilipo kaburi lake ndipo walipoambiwa kuwa mwanamke huyo yupo nchini Canada.
No comments:
Post a Comment