Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Monday, 24 July 2017

MAGUFULI:NIMEJITOLEA KUFA AU KUPONA MPAKA NIHAKIKISHE MALI ZA WATANZANIA WANYONGE HAZIIBIWI



Rais Dkt. John Pombe Magufuli ‘JPM’ amesema yeye kama kiongozi mkuu wa nchi haogopi vitisho vya kufungwa ama kushtakiwa vinavyotajwa na baadhi ya wanasiasa baada ya
kuwashughulikia wawekezaji wanaokiuka mikataba na kuhujumu uchumi wa nchi na badala yake ataendelea kuwatetea Watanzania
wanyonge ili wapate haki yao.

Raid Magufuli ameyasema hayo jana wakati
akiwahutubia wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini humo.

“Hii nchi imejaa mafisadi, wamo wa CCM, Chadema, CUF, ACT, wazungu na wengine hawana chama.

"Siogopi kufungwa, kama mliniteua niwatetee, nitawatetea kwa nguvu zangu zote juu ya majizi, tumeibiwa vya kutosha, madini yetu
yanachimbwa yanapelekwa nje na hatupati kitu.

“Wengine wamelipwa pesa ili kupinga tusichukue hatua dhidi ya majizi, nawaambia mimi kama rais nimejitoa kufa na kupona mpaka nihakikishe mali za Watanzania wanyonge haziibiwi na haki yao wanaipata.

No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post