Waziri mkuu Kasssimu Majaliwa amesema safari ya Watanzania kuhachana na nguo za mitumba imewadia kutokana na uwepo wa viwanda vya kutengeneza nguo nchini.
-Aidha, Waziri Majaliwa amewapa matumaini wakulima wa pamba na kusema hawana sababu ya kwenda kuuza nje ya nchi na badala yake wauze pamba hiyo katka viwanda vya ndani ili vizalishe nguo za kutosha zitakazouzwa nchini kwa gharama nafuu.
"Pamba yote inaweza kuchakatwa nchini, hivyo hakuna haja ya kuiuza nje ya nchi. Natoa wito kwa wakulima wetu wa pamba walime mazao ya kutosha kwa sababu soko la uhakika lipo na hii ndiyo safari ya mwisho ya mitumba Tanzania" alisema Waziri Mkuu
Waziri Mkuu aliasema hayo jana wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Namera kilichoko Gongo la Mboto na kiwanda cha nguo cha Nida kilichopo Ubungo Dar es Salaam ambapo alidai viwanda vya kutengeneza nguo nchini ni ushahidi tosha kwamba nchi iko njiani kuondokana na matumizi ya nguo za mitumba kwa kuwa nguo nyingi zitakuwa zinatengenezwa nchini, hivyo kupatikana kwa bei nafuu.
Mbali na hilo Waziri mkuu alitoa wito kwa wamiliki wa viwanda vyote nchini kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi waishio katika maeneo ya karibu na viwanda hivyo sambamba na kulipa kodi kwa wakati na kwa viwango sahihi.
Kwa mujibu wa Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu Mh, Jenista Mhagama alisema kuwa Tanzania imeazimia kufika mwaka 2018 kuhachana na biashara ya kuingiza nguo za mitumba kutoka nje, makubaliano ambayo yalifikiwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Chanzo:Eatv
No comments:
Post a Comment