Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Thursday, 13 July 2017

UPADRE:MCHEZAJI WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED AWA PADRE

Aliyewahi kuwa mchezaji wa Manchester United apewa Daraja ya Upadre

Tarehe 08 Julai 2017 Kanisa la Northern Ireland lilipata padre mpya. Fr Philip Mulryne aliyepata kuwa mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Manchester United. 
Fr Philip  amepewa daraja ya upadre katika Shirika la Wadomisiani (Domician Order)

Father Mulryne, ambaye ameripotiwa kuwa alikuwa akipokea kiasi cha Euro 600,000 kwa mwaka ameweka nadhiri ya Ufukara. Philip amepewa daraja hilo na Askofu Mkuu wa Dublin Joseph Augustine Di Moia ambaye amesafiri kutoka Roma kwa ajili hiyo. Fr Mulryne aliweka nadhiri na kuwa Shemasi Oktoba mwaka 2016.  

Katika maisha yake ya michezo,  Fr Philip  alifanikiwa kujiunga na timu ya Manchester United mwaka 1997 baada ya kuonesha kipaji katika timu za vijana na pia kuichezea timu ya Taifa ya Northern Ireland 
Alistaafu rasmi soka mwaka 2009 na akaanza safari yake kuelekea wito wa upadre na akajiunga Seminari. 
Miaka miwili alisoma masomo ya Filosofia katika chuo cha Queen's University cha Belfast na Maryvale Institute kabla ya kujiunga na Pontifical Irish College Roma kwa ajili ya masomo ya Theolojia kwa mwaka mmoja katika Chuo Kikuu cha Gregorian.

Alijiunga katika Nyumba ya Unovisi mjini Cork mwaka 2012 na kupadrishwa mwaka 2017.




No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post