Waziri wa zamani wa nisharti na madini na mbunge wa jimbo la Sengerema, William Ngeleja amerejesha rasmi Serikalini fedha alizopokea kutoka kwa James Rugemalira mnamo tarehe 12/02/2014 katika mgao wa Escrow ambazo ni kiasi cha shillingi milioni 40.4 ili kukwepa kuendelea kuandamwa na kashfa hiyo
Ngeleja amesema kuwa "Nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa tu, kwa sababu sitaki kuwa sehenu ya kashfa/tuhuma hizo" Ngeleja.
'Leo nina zaidi ya miaka 12 nikiwa kiongozi wa Umma lakini sijawahi kukumbwa na kashfa ya rushwa au ufisadi.
Kwa vile sasa imedhihirika kwamba aliyenipa msaada huu anatuhumiwa kwenye kashfa ya akaunti ya ESCROW nimeamua kuchukua hatua.
Kupokea msaada ni jambo la kawaida, ila ikibainika kuna harufu ya uchafu hata kama haujathibitshwa na vyombo husika ni vyema kujiepusha nao.
Nimerudisha fedhan hizi ili kulinda maslahi ya nchi yangu na heshima ya chama changu,Serikali,wanasengerema, familia yangu na heshima yangu.
Nimepima na kutafakari, na hatimaye nimeamua, kwa hiari yangu mwenyewe, kurejesha kiasi cha milioni 40.4 serikalini.
No comments:
Post a Comment