HII NI SEHEMU YA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI ALIYOITOA LEO TABORA MJINI
Rais Magufuli: Tabora Hoyee....
=>Mh mkuu wa mkoa wa Tabora, waziri wa ujenzi, waziri wa maji, naibu waziri wa afya Dr Kigwangala, wabunge wa Tabora, MaDC, viongozi wa dini, waheshimiwa madiwani, wakurugenzi, waandishi wa habari, wanachuo, viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
=>Kwanza ninawashukuru sana kwa heshima kubwa mliyonipa na kwa kumtanguliza Mungu na kwa kunichagua. Asanteni sana kwa kura nyingi mlizonipa. Mungu awabariki sana.
=> Niseme kwa dhati kwa jinsi mlivyonipa kura nyingi na wabunge na madiwani, napenda niseme nina deni kubwa.
=>Tabora ina heshima kubwa katika kutetea ukombozi wa taifa letu.
=>Ndugu zangu wa Tabora, nimesema mkoa wa Tabora una heshima ya pekee. na ndiyo maana wananchi wa Tabora niliwaomba kwa heshima kubwa.
=>Nilipochaguliwa na ndiyo maana nimekuja hapa kuwashukuru na kuzindua miradi ya maedeleo.
=>Namshukuru sana rais wa awamu ya nne. Miradi ninayowezindua leo ilianza awamu ya nne. Mimi nilikuwa waziri wake. Tutakuwa tumekosa shukrani bila kushukuru Kikwete.
=>Ninafahamu, miradi ya ujenzi iliyopo katika manispaa ya Tabora. Ukiangalia fedha zilizotumika pale fedha zote zilitolewa na serikali.
=>Kwa juhudi hizi kubwa zinazofanywa na serikali, Kuna fedha zilizotolewa na benki ya dunia kwa ajili ya kujenga barabara. Na leo nimetoa maagizo, uwanja wa ndege upanuliwe.
=>Tunafanya yote haya ili wananchi wachague wenyewe, watatumia usafiri gani wanapotaka kusafiri.
=>Ndugu zangu wanatabora tutembee kifua mbele. Na leo mmeshuhudia Prof Mkumbo
=>Na mimi nitaendelea kuchomoa wale wenye akili waliopo kwenye vyama vingine, wale vilaza wataendelea kubakia kwenye vyama vingine.
=>Maana mimi ni rais wa wote, hata ukiwa chadema mimi kwangu sawa tuu, ukitaka ninyooshe vidole; si vidole tuu..
=>Reli tuliyonayo ilijengwa mwaka wa 1905 na kuja kumaliziwa na wajerumani.
=>Kwahiyo tunajenga reli ya umeme, na itakuwa inachukua muda mchache tuu.
=>Niwaombe wana Tabora.
=> Sisi wanasiasa tuache siasa katika maendeleo.
=>Nimekuwa nabomoa nyumba ili zipite barabara wakati nikiwa waziri lakini bado mlinichagua.
=>Watu walio katika hifadhi ya reli tutabomoa ili wasitucheleweshe, na waanze kujiandaa kutafuta maeneo.
=>Kwa mujibu wa sheria namba ya 4 na 5 kifungu cha tatu, watu watakaobomolewa watalipwa.
=>Tunataka hiyo njia ya reli iwe nyeupe, haya ndiyo maendeleo tunayotaka.
=>Nimesikia kilio cha mbunge wa hapa, najua lazima aseme hivyo maana mmemtuma awasemee.
=>Tabora ni miongoni mwa mikoa yenye matatizo ya maji.
=>Tuliahidi kwenye ilani ya uchaguzi kwamba maji vijijini 85% na mijini 95%
=>Waziri mkuu wa India alipokuja kututembelea, nilimuonyesha Tabora kuwa ndiyo kipaumbele katika mradi wa maji ambao utauhusisha vijiji 89.
=>Leo nimeweka jiwe la msingi na ndani ya miaka 2, mradi ule utakuwa umekamilika.
=>Wananchi wa Tabora mmependelewa, ninawaomba sana tushirikiane na tuvumiliane. Mambo yote hayawezi kufanyika siku moja.
=>Tumemaliza barabara zote. Na huo ndio utanzania. Ipo mikoa ambayo haijapata barabara. Umeme nao utaletwa, mtuvumilie.
=>Wananchi tulipe kodi, kwa wananchi wa kawaida mnalipa kodi. Watu wanaokwepa kodi ni wale matajiri wakubwa.
=>Na ninyi wananchi wa Tabora muendelee kuwaelimisha wananchi wengine umuhimu wa kulipa kodi.
=>Tumechukua hatua ya kukusanya mapato kutoka bilion 800 hadi trilioni 1.3.
=>Mwaka jana tuliongeza wanafunzi waliopata mikopo kutoka 98,000 hadi 125,000
=>Tumetangaza ajira kwa madaktari na manesi.
=>Tulikuwa tumejaza wafanyakazi hewa kila sehemu.
=>Ni Tanzania tuu kila sehemu unakuta kila kitu hewa, kuna mpaka wakimbizi hewa.
=>Kumekuwa na wanafunzi hewa 65,000. Kumekuwa na mikopo hewa ya zaidi ya bilioni 3. mikopo hewa ya zaidi bilioni 38. Kulikuwa na kaya hewa.
=>Hizi fedha zilitakiwa ziende kwenye hospitali, zinunue ndege na kwa wafanyakzi tutaanza kutoa promotion.
=>Kwa Tumbaku, tutaanza kuchukua hatua.
=>Na kwa ombi la viwanda niwaombe wabunge walete wawekezaji waje wajenge viwanda na serikali itawapa support. Na tutampunguzia hata ushuru, tutampa hata eneo.
=>Tushikamane wote wabunge wa Tabora, na kukiwa na kiwanda Tabora hata hili tatizo la Tumbaku tutalimaliza.
=>Nimekuja hapa kuwashukuru, nawashukuru sana wabunge wa Tabora, wana ushirikiano sana.
=>Tumepunguza tozo za mazao kwa mzigo usiozidi tani moja.
=>Kwenye mifugo tumefuta tozo saba na uvuvi tozo 5.
=>Kwa wafanyabiashara wadogo, watapata utambulisho maalumu na wapewe maeneo.
=>Mh Bashe amezungumza kuhusu wizi uliokuwa unafanywa katika dhahabu.
=>Na kutumbua nitaendele kutumbua na wala siogopi.
=>Na ndiyo maana nilipoingia nilifuta safari zote, semina semina zote nilifuta. kama unataka kufanya semina, fanya hata chini ya mwembe.
=>Kwa hiyo nimebinya hiyo mianya ya wakubwa, nikawapa wananchi.
=>Wafanyakazi wamekuwa hawalipwi, wamekuwa wanacheleweshewa na tumeamua madai ya watumishi lazima yalipwe mara moja.
=>Tunafanya hivi kwa maslahi ya wananchi hasa wananyonge, hii ndiyo Tanzania ninayoitaka.
=>Maendeleo hayawezi kupatikana bila ya kuwepo amani.
=>Katika mikoa hii ya Tanzania, nimeteua viongozi wengi, hawa wote wapo kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi.
=>Niwaombe viongozi wa mkoa wa Tabora mshughulikie kero za wananchi.
=>Inawezekana viongozi mnakaa sana ofisini bila kutatua kero za wananchi.
=>Niwaombe viongozi wakuu wa mkoa, wakuu wa wilaya msikilize kero za wananchi na kuyatatua.
=>Sasa nitakuwa natembea mikoani, nikiona kero ambazo wakuu wa mikoa na wilaya wangeweza kutatua, nitalala nao mbele.
=>Najua hapa mkoa wa Tabora, kuna tatizo kubwa la ardhi. Ninaomba mkuu wa mkoa kila mwenye tatizo, uelekeze litatuliwe na nani. Yale ambayo yamekushinda ukiona kwangu ni mbali sana mpelee waziri mkuu wangu.
=>Nipende kuwaomba mshirikiane na wabunge wenu na madiwani.
=>Mimi nipo pamoja na ninyi na mapokezi niliyoyapa hapa Tabora yananifanya niwe na deni kubwa.
=>Ninawashukuru sana walioniombea hapa, niwashukuru sana wana Tabora.
Niwashukuru sana na Mungu awabariki Tanzania.
HII NI SEHEMU YA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI ALIYOITOA LEO TABORA MJINI
Reviewed by
Unknown
on
July 25, 2017
Rating:
5
No comments:
Post a Comment