MAGUFULI AKUMBUKA: Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuonyesha Mkewe Mama Janeth Magufuli kitanda alichokuwa akitumia kulala wakati akisoma kidato cha tatu katika shule ya seminari katoke iliyopo Biharamulo Mkoani Kagera.
Dkt Magufuli amemweleza mkewe kuwa alivunja hilo dirisha na mpaka leo halikutengenezwa ambapo leo hii amekabidhi kiasi cha shilingi milioni moja ili kukarabati dirisha na madirisha mengine ya shule hiyo.
Dkt Magufuli yupo mkoani Kagera kwa ziara ya siku mbili mkoani humo.
Picha/Ikulu, Tanzania.
CHANZO: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment