Baraza Kuu la Uongozi CUF (Linalomuunga Mkono Prof. Ibrahim Lipumba), limewavua uanachama Wabunge 8 wa Viti Maalum na Madiwani 2 wa chama hicho kwa kosa la kukisaliti chama.
Hapo jana Wabunge 10 na madiwani wawili wa CUF, waliiitwa kwa ajili ya mahojiano katika ofisi za Chama cha Wananchi (CUF) hadi saa 5.00 walikuwa bado hawajaonekana kwenye ofisi hizo.
Wabunge hao wanaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad waliitwa ili kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho kuhusu mgogoro unaoendelea ndani ya CUF.
No comments:
Post a Comment