Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Sunday, 2 July 2017

BARRACK GOLD CORPORATION:Kampuni yenye historia ya migogoro Duniani

Eneo la Machimbo ya dhahabu Pueblo Viejo la Kampuni ya Barrack Gold Corporation, moja ya machimbo makubwa linaonekana katika mji wa Cotui katika Jamhuri ya Dominica huko Carribean.

Mapema mwaka huu serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ilianza kutilia mashaka utendaji wa makampuni ya uchimbaji madini nchini hasa baada ya kuaminika kuwa kiasi kisichojulikana cha mchanga wenye madini kinatolewa nje ya nchi bila udhibiti mzuri.

Serikari ya Rais John Joseph Pombe Magufuli iliunda tume ya uchunguzi kufuatilia suala hilo na mwezi uliopita matokeo ya uchunguzi huo yalionyesha kuwa Tanzania imekoseshwa mabillioni  ya mapato kutokana na mauzo ya madini ya mchanga unaotolewa nje na makampuni hayo.

 Moja ya kampuni kubwa iliyomulikwa katika mgogoro huo ilikuwa Acacia ambayo kampuni yake mama ni Barrick Gold Corporation yenye makao yake makuu nchini Canada. Barrick Gold ni moja ya kampuni kubwa sana za  uchimbaji madini duniani ikiwa inaendesha uchumbaji madini katika mabara yote ya dunia.

Rais Dr John Magufuli na Mwenyekiti  wa kampuni ya Barrick Gold Corporation Prof John L. Thornton. Ambao ni wamiliki wa Acacia Gold Minning.

Sasa imedhihilika kuwa kampuni hiyo imekuwa ikikabiliwa na matatizo ya kimikataba na mwenendo mbaya wa shughuli za uzalishaji katika nchi kadha ambako kampuni hiyo ina machimbo ya madini.

Katika uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la nchini Amerika {VOA} unaonyesha kuwa nchi nyingi katika mabara ya Asia, Afrika na Amerika ya Kati zimekuwa na migogoro ya kimikataba na madai ya uharibifu wa mazingira dhidi ya Barrick Gold. Pia kumekuwepo na madai ya udhalilishaji wa wafanyakazi katika machimbo yanayomilikiwa na Barrick Gold. Japo kwa hapa nchini hakuna madai hayo labda sababu ya husiri huliopo katika migodi inayo milikiwa na kampuni hiyo hapa Tanzania.

Kama ambavyo serikali ya  Tanzania imetaka mikataba na makampuni ya madini- ikiwemo Acacia-irejewe upya na kufanyiwa marekebisho, serikari ya Jamhuri ya Dominica nayo inadai kuwa mikataba kati yake na Barrick Gold ina athari mbaya kwa taifa hilo la Caribbean.

Idara ya forodha nchini Dominica imetuhumu Barrick Gold kwa ''mwendelezo wa kukiuka utaratibu wa kukamilisha kujaza fomu za kusafirisha nje madini ya dhahabu.''

Mwaka 2009 gazeti la This Day la hapa Tanzania liliripoti madai kwamba kampuni ya Barrick Gold lilihacha kemikali zinazotumika katika uchimbaji kuchanganyika na vyanzo vya maji katika mkoa wa Mara na hivyo kutishia maisha ya wakazi wa mkoa huo.

Huko nchini Pakistan mwaka 2012 mahakama ya juu ilibatilisha hati ya kukodisha aridhi waliyo pewa Barrick na kampuni nyinyinge ya Madini Antofagasta ya nchini Chile. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, hatua hiyo ilifuatia madai kuwa eneo hilo lina dhahabu na shaba nyingi kuliko sehemu yoyote duniani. Kampuni hizo zikafungua mashauri katika kesi ya upatanishi ya kimataifa na mpaka leo mgogoro huo haujatatuliwa.


Mwaka 2009 gazeti la the star, la Toronto, Canada liliripoti  kuwa  wakati Barrick iliponunua Placer Dome, iliridhi mgogoro uliokuwepo muda mrefu katika eneo la uchimbaji la Porgera Valley, Mwaka 2006 Gazeti hilo hilo lilieleza mgogoro huo kuwa kama ni "eneo la kivita, ambapo mamia ya wanakijiji  walikuwa wamekabiliwa na walinzi wa mgodi zaidi ya 400 na polisi katika ugomvi uliopelekea umwagaji damu" ambao ulisababisha watu wanne kuuawa.

Mwaka 2003 taarifa iliyotolewa na taasisi ya haki haki za binadamu, Lake Cowel Campaign ya Sydney, Australia ilidai kuwa sumu iliyovuja katika ngome ya machimbo ya Barrick huko Australia Magharibi ambayo Barrick ni mshirika.

Nchini Argentina gazeti la IPS news la Santiago liliripoti kuwa Barrick ililazimika kusitisha mpango wa kuchimba dhahabu katika Mlima Famatina kwenye jimbo la La Rioja kufuatia maandamano yaliyofanywa na jamii nzima na kashfa ya ufisadi iliyomuhusisha gavana wa jimbo ambaye alikuwa anausahidia mradi huo. Polisi walilipotiwa kuwashambulia waandamanaji.


Chanzo cha habari cha La Republica nchini Peru kililipoti uvunjifu wa sheria ulitokea Peru mwaka 2006 wakati waandamanaji wakidai mazingira bora ya kazi katika eneo la machimbo ya Barrick huko Pieriana, yalipopelekea watu wawili kupoteza maisha katika mikono ya polisi.


Nchini Marekani pia tangu Barrick ilipochukua machimbo makubwa ya Goldstrike na eneo la kuchenjua madini katika jimbo la Nevada miaka 1980 kumekuwa na malalamiko kuhusu  athari za operesheni zao kwa mazingira. Mwaka 2005 gazeti la New York Times lilichapisha  habari ukurasa wa mbele ikitumia kigezo cha machimbo hayo jinsi yanavyo athiri kwa kiwango cha juu matatizo ya maji yanayo sambazwa na serikali wakati kampuni hiyo ikizalisha sumu zinazotokana na mabaki ya mercury kuliko kiwanda chochote kingine.






CHANZO: VOA 























































































































No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post