Kampeni za wagombea Urais watatu zimeanza rasmi leo nchini humo ambapo kura zitapigwa kuanzia tarehe 5 Agosti mwaka huu.
Rais Paul Kagame naye amejitosa kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine tena na kwa awamu hii uchaguzi huu umeonekana kuwa na upinzani mkali ukilinganisha na kipindi kilichopita.
Wagombea pekee wanaogombea urais mwaka huu ni Paul Kagame wa chama cha Rwanda Patriotic Front (RPF-Inkotanyi); Frank Habineza wa Democratic Green Party of Rwanda na mgombea binafsi, Philippe Mpayimana.
Chanzo: Rwanda news
No comments:
Post a Comment