ALIYEOMBA WATU WASILIE ILA WAMUOMBEE MUMEO NAYE AFARIKI, WAZIKWA PAMOJA
Mwanamke mmoja mjini Moshi amefariki dunia siku moja kabla yamazishi ya mumewe.
Tukio hilo limekuwa gumzo katika Kata ya Pasua na viunga vyake kwa kuwa mwanamke huyo ndiye aliyekuwa akiwasihi waombolezaji
wasilie bali wamuombee mumewe.
Damian Matemba, mfanyabiashara anayemiliki duka la vifaa vya ujenzi na huduma ya miamala ya fedha, alifariki dunia Julai 19 na mkewe, Taudensia akafariki juzi.
Maziko ya Matemba yalipangwa kufanyika leo, Julai 25 na mkewe alishiriki hatua zte a msiba huo lakini naye aliugua ghafla na kufariki dunia.
Hali ya simanzi ilitanda katika ibada ya kuwaaga marehemu hao leo illyofanyika katika Kanisa Katoliki, Kigango cha Pasua.
Juma Raibu, ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Kilimanjaro, akizungumzia msiba huo amesema umewagusa sana.
Raibu ambaye ni jirani wa marehemu hao, amesema si jambo la kawaida kwa wanandoa kufariki na baadaye kuzikwa pamoja.
ALIYEOMBA WATU WASILIE ILA WAMUOMBEE MUMEO NAYE AFARIKI, WAZIKWA PAMOJA
Reviewed by
Unknown
on
July 25, 2017
Rating:
5
No comments:
Post a Comment