MIZIGO YA BURUNDI NA DRC SASA KUHUDUMIWA KIGOMA (VIF KIGOMA)
Leo nimekuwa na mkutano mzuri Sana wa Central Corridor hapa Kigoma katika Hoteli ya Lake Tanganyika. Mkutano huu unaohusisha watendaji wakuu wa Mamlaka za Bandari, Reli na Barabara wa Nchi za Tanzania, Burundi na DR Congo. Pia wafadhili wa Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Africa na Trademark East Africa ( John Ulanga inakuhusu ).
Washiriki wengine ni Makatibu Wakuu wa Wizara za Uchukukuzi wa Nchi za Mamlaka ya Ziwa Tanganyika na Wafanyabiashara.
Mkutano umependekeza kuwa Mizigo yote kupitia Bandari ya Dar Es Salaam inayokwenda Burundi na Mashariki ya Kongo ishughulikiwe hapa Kigoma. Kitaalamu mizigo itakuwa CIF Kigoma na hivyo Wafanyabiashara wa nchi Hizo hawatakuwa wanakwenda Dar kufuata mizigo yao bali hapa Kigoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Kakoko ameahidi kusimamia utekelezaji wa pendekezo hili haraka ndani ya Mwaka huu wa Fedha.
Hili pendekezo litasaidia Sana kukuza Uchumi wa Kigoma. Nachukua fursa hii kuwataka wananchi wa Kigoma kujiandaa Kwa fursa kubwa za ajira kutokana na uamuzi huu. Hadhi ya Kigoma kuwa Mji wa Biashara Kama ulivyokuwa wakati tunakua Sasa inarudi. Bandari ya Dar hupitisha tani 1.7m za mizigo kwenda DRC na tani 350,000 kwenda Burundi.
Pendekezo hili pia litasaidia Sana Kwenye mradi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wa Ujiji City- The Great Lakes Trade and Logistics Center Kwa kupunguza gharama za kuagiza mizigo na muda wa mizigo kukaa Bandarini Dar.
Pia imeonekana ni vizuri Tanzania kuachana na mfumo wa Single Customs Territory kati yake na DRC ili kurudisha Biashara ya Usafirishaji kwenye Bandari ya Dar Es Salaam. Ninaunga mkono jambo hili kwani litawezesha kazi za watu wetu kurudi na kukuza sekta ya usafirishaji nchini.
Zitto Kabwe
Kibingo, Mwandiga Township
Kigoma
27/7/2017
MIZIGO YA BURUNDI NA DRC SASA KUHUDUMIWA KIGOMA (VIF KIGOMA)
Reviewed by
Unknown
on
July 27, 2017
Rating:
5
No comments:
Post a Comment