Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Monday, 31 July 2017

JAMHURI YA MUUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


     TAARIIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Majadiliano kati ya Kamati Maalum ilivoundwa na Rais Wa Jamhuru y Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Wawakilishi
kutoka Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hivo hapa nchini yameanza leo tarehe 31 Julai, 2017 Jiini Dar es Salaam.

Kamati Maalum ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba Prof.
Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi na Kamati ya kutoka Barrick Gold Corporation inaongozva na Afisa Mwendeshaji Mkuu Bw. Richard Williams.

Akizungumza kabla ya kuanza kva majadiliano hayo Prof. Kabudi amesema kuwa kamati yake imejipanga vizuri kujadiliana na Barick Gold Corporation juu ya madai ya Tanzania katika biashara ya madini ya kampuni hiyo hapa nchini na itahakikisha inasimamia maslahi va Tanzania ipasavvo.

Kwa upande wake Bw. Richard Williams ameshukuru kuwepo kwa majadiliano hayo na amesema Kampuni ya Barrick Gold Corporation
imeyapokea madai ya Tanzania kva mtazamo chanya na ipo tayari kujadiliana
na kufikia makubaliano yenye maslahi kwa pande zote mbili.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano va Rais, IKULU
Dar es Salaam
S1 Julai, 2017

KASSIM MAJALIWA: "NAAGIZA KUKAMATWA KWA ALIYEKUWA MEYA WA MBEYA"

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mbeya Bw. Emanuel Kiabo kumkamata na kumuhoji Mheshimiwa Atanas Kapunga aliyekuwa Meya wa Jiji la Mbeya na wenzake 11 kwa tuhuma za kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 63.448.

“Serikali hii haiwezi ikawaacha watu hawa ambao wameisababishia hasara kubwa kiasi hiki tena kwa halmashauri moja. Kama wako humu ndani nagiza wakamatwe na waanze kuhojiwa na ambao wamestaafu au kuhamishwa kituo cha kazi wasakwe popote walipo ili nao waje kuhojiwa.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Julai 31, 2017) alipozungumza na watumishi wa Halmashauri za wilaya ya Mbeya na Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Benjamin Mkapa.

Wengine ni waliowahi kuwa wakurugenzi wa Jiji hilo ambao ni Bw. Mussa Zungiza, Bi. Elizabeth Munuo, Bw. Juma Idd na Dkt. Samwel Lazaro aliyekuwa akikaimu nafasi ya Ukurugenzi.

Aliyekuwa Mweka Hazina wa Jiji, Bw. James Jorojik pamoja na waliokuwa wajumbe wa Bodi ya Zabuni ambao ni Bw. Mussa Mapunda, Bw. Samweli Bubengwa, Bw. Davis Mbembela, Bi. Lydia Herbert na Bw. Bernard Nsolo ambao walipitisha nyongeza ya mradi huo bila ya kuzingatia maslahi ya Jiji pamoja Emily Maganga ambaye hakuishauri vizuri bodi hiyo.

Sunday, 30 July 2017

MWANZILISHI KAMPENI YA 'MAGUFULI BAKI' AKIMBILIA TCRA

Mmalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeombwa kufuatilia kwa makini  mawasiliano ya simu za mkononi ili kubaini watu wanaotumia mitandao hiyo  kinyume na sheria.

Ombi hilo limetolewa na mwanaharakati Lawrence Mabawa  jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari vitisho anavyopata kupitia simu ya mkoni baada ya kutambulisha kampeni yake ya ‘BAKI MAGUFULI’.

Kwa mujibu wa Mabawa, baadhi ya wananchi wameelewa vibaya kampeni hiyo na kufikia hatua ya kutoa maneno ya matusi na kejeli kwake.

Akifafanua lengo la kampeni yake, Mabawa amesema alimaanisha  kuwa Rais abaki na msimamo wake ambao kwa kiasi kikubwa unapeleka taifa la Tanzania mbele kimaendeleo, na si kama ambavyo watu hao wameichukulia.

HAJI MANARA AMKABIDHI JPM KIWANDA KIKUBWA ZAIDI

Mkuu wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amemuonesha Rais Magufuli kiwanda kingine ambacho amedai kuwa ni kikubwa kuliko viwanda vyote nchini kinachoweza kusaidia utekelezaji wa kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga Tanzania ya viwanda.

Kiwanda hicho ni mchezo wa soka, ambapo Manara amesema endapo kitafanyiwa uwekezaji wa kutosha kitaweza kuzalisha ajira nyingi kuliko viwanda vyo ambavyo serikali ya awamu ya tano imepanga kuvijenga na kuviendeleza.

“TFF wanatakiwa waje na mpango wa kukiboresha na kukiunda kiwanda hiki sasa, maana mimi naona kama vile kiwanda hiki hakipo, serikali iwekeze kwenye football kuanzia chini. Kama Rais ameingia mahali, nchi nzima inatumia mashine za EFD, TRA makusanyo yameongezeka, ofisini kuna nidhamu ya kazi kwenye taasisi za umma, mambo yanakwenda, nakuhakikishia Rais akiingia hapa kwenye mpira, akaja kutuundia hiki kiwanda, ataacha legacy ambayo hajaacha Rais yeyote, na kisiasa itamsaidia sana katika uchaguzi wa 2020, kwa sababu hakuna kitu kinachopendwa zaidi katika nchi hii kama mpira” Amesema Manara.

Je, wewe unasemaje?

"Uwoya alinitaka mwenyewe" - Msami Baby.

Mwanamuziki anayefanya poa na ngoma ya 'So Fine' Msami baby amedai hana mawazo ya mpenzi wake wa zamani, msanii wa bogo movie, Irene Uwoya kutoka kimapenzi na msanii Dogo Janja kwani hakuwahi kumtaka bali mwanadada huyo ndiye aliyemtaka wa kwanza.

Msami amefunguka hayo kwenye FNL ya EATV ijuma hii wakati alipokuwa akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho kuhusu kupotea kwake kwenye game kama kumechangiwa na mawazo ya mapenzi.

"Dogo Janja kutoka kimapenzi na Irene haijanishangaza au kunifanya mimi nipotee kwenye game kwa sababu kwenye mapenzi mimi sijawahi kuachika bali huwa naachagaUwoya yeye ndiye alinitongoza mimi kwani sijawahi kumtongoza ........". Kuhusu kuwa kimya ukweli nilipata ajali ya kuvaana na gari uso kwa uso kwa hiyo nilikuwa najiuguza kwanza, Ajali yangu haikusababishwa na 'stress' za mapenzi kabisa". Msami baby alifunguka.

Msami baby aliwahi kutajwa miaka miwili nyuma kujihusisha kimapenzi na diva huyo wa bongo movie huku akidaiwa kumtelekeza mpenzi wake na baada ya hapo pia alitajwa sana kujiweka kwenye mapenzi na muigizaji Kajala

HALI MBAYA YA UPATIKANAJI, USAMBAZAJI NA UGAWAJI WA PEMBEJEO KWA WAKULIMA WA KOROSHO

Leo chama chetu kimetoa 'Taarifa juu ya Hali Mbaya ya Upatikanaji, Usambazaji na Ugawaji wa Pembejeo kwa Wakulima wa Zao la Korosho Nchini'. Hali mbaya ambayo inatishia sekta nzima ya korosho nchini (zao linaloingiza fedha nyingi za kigeni kuliko mazao yote ya bishara nchini).

Ili nchi kama yetu iendelee tunahitaji ukuaji wa kilimo (sekta inayoajiri 65.5% ya watanzania wote) kwa kiwango cha 10% kwa miaka mitatu mfululizo, kisha ukuaji wa 6% kwa miaka mingine 10. Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani ukuaji wa umedumaa zaidi, kwa mwaka jana kilimo kikikua tu kwa 0.6%, lakini uzalishaji wa korosho ulikuwa kwa zaidi ya 70%, wakulima wa korosho, hasa watu wa kusini, mlilifuta machozi taifa, mkituingizia fedha za kigeni zaidi ya Dola milioni 340. Inasikitisha sana kwamba Serikali sasa inataka kuwafukarisha, haithamini mchango wenu huu.

Taarifa tuliyotoa leo inahusisha utafiti uliofanywa na Viongozi wa chama cha ACT Wazalendo wa ngazi ya Majimbo katika mikoa mitano ya Lindi, Mtwara, Pwani, Ruvuma na Tanga kupitia mazungumzo yao na wakulima wa korosho katika mikoa hiyo mitano inayolima korosho zaidi nchini kutafiti hali ya upatikanaji, usambazaji na ugawaji wa pembejeo.

Nafarijika mno kuongoza chama cha namna hii, chama kinachojikita katika kuzungumzia masuala ya watu, chama kinachpinga pale inapostahili kupinga na kinachotoa sera mbadala za namna ya kuendesha masuala mbalimbali ya nchi.

Nakushukuru sana Katibu wa Itikadi, Mawasiliano ya Umma na Uenezi wa ACT Wazalendo kwa kuongoza jopo la Viongozi wa majimbo kufanya majadiliano haya na wananchi, nawashukuru viongozi wote wa majimbo mlioshiriki zoezi hili, mmefanya kazi kubwa sana.

Kwa wakulima wote wa Korosho nchini, mchango wenu ni mkubwa mno kwa Taifa hili, wakati huu ambao Serikali inataka kuharibu maisha yenu, zaidi ya Wakulima 600,000, pamoja na familia zenu, ACT Wazalendo itasimama nanyi, itapaza sauti kusemea matatizo yenu, na itayawakilisha mawazo yenu juu ya namna ya utatuzi wa kadhia yenu, hatutawaangusha kwenye hili.

' Achimbuzanga Aiche' (marafiki zenu wamekuja). Tutakuwa pamoja.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Julai 30, 2017

HUU NDIO UFAFANUZI WA NEC KUHUSU UTEUZI WA WABUNGE CUF

Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) kufuatia uteuzi wa wabunge wa viti maalum wa chama hicho, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi dhidi ya uteuzi huo.

Imesema kuwa imesikitishwa na kushangazwa na taarifa ya Baraza la Kuu la Taifa la chama hicho kusema kuwa tume hiyo imekiuka kanuni zake katika uteuzi wa wabunge wanane wa chama hicho ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi hivi karibuni na wabunge waliofukuzwa uanachama.

Aidha, NEC imesema kuwa chama husika kilipewa fursa ya kupendekeza majina kabla ya tume hiyo kuanika hadharani majina ya wabunge hao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima kujibu tuhuma zilizotolewa na CUF na kusambazwa katika mitandao ya kijamii, imesema kuwa katika kanuni iliyojiwekea NEC katika uteuzi wa watu wa kujaza nafasi hufuata mpangilio wa majina.

“Chama husika ndicho huwa kinajua ni nani siyo mwanachama wa chama hicho kwa kipindi cha kujaza nafasi zilizoachwa wazi inapokuwa imetokea lakini siyo tume, hivyo malalamiko kutoka Baraza Kuu la Taifa CUF, yanashangaza,”amesema Kailima.

Hata hivyo, Kailima amesema kuwa taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikihusisha NEC kukihujumu chama hicho si za kweli na zinalengo la kupotosha jamii katika utekelezaji wa kazi za Tume.

Saturday, 29 July 2017

Uturuki yaomba msaada Tanzania

Tanzania imeombwa kuisaidia Uturuki kiwango cha Tani 20 ya Korosho kufuatia nchi hiyo kuwa na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo yenye uhitaji zaidi nchini Uturuki.



Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara kutoka Uturuki ijulikanayo kama 'Turkish Exportetrs Assembly' (TIM) Bwana Kemal Batuhan Yazici amesema kuwa, kiwango cha korosho kilichopo nchini kimeshuka wakati mahitaji ya nchi ni Tani 20, hivyo wanaitegemea Tanzania kuondoa uhaba huo nchini mwao.
Kemal Batuhan Yazici amesema, Korosho inayohitajika nchini Uturuki ni ile ambayo tayari imechakatwa na kufungwashwa vyema kwa viwango vya kimataifa na sio malighafi hivyo ni vyema wafanyabiashara hiyo wakaandaa utaratibu wa haraka kuhakikisha Korosho zinasafirishwa kutoka Tanzania kwenda nchini Uturuki.
Kwa muda wa miezi sita, kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Uturuki kimeongezeka kwa asilimia 9 kwa bidhaa za Tanzania zinazosafirishwa kutoka nchini Tanzania kwenda nchini Uturuki hivyo ongezeko hilo linaashiria Tanzania kupata soko lenye tija nchini Uturuki.

Katika siku za hivi karibuni nchi ya Uturuki imeongeza ushirikiano wake wa kibiashara na nchi ya Tanzania ambapo nchi hizo zimepata fursa mara kadhaa kuonesha maeneo yao ya uwekezaji baina yao ili kuongeza faida na kuleta maendeleo.

MAKAMU WA RAIS WA KENYA AVAMIWA NYUMBANI KWAKE NA WATU WENYE SILAHA



Watu wenye silaha wamevamia Nyumbani kwa Naibu wa Rais William Ruto eneo la Sugoi Kaunti ya Uasin Gishu tkribani kilomita 420 kutoka mji mkuu Nairobi.

Hadi sasa vyombo vya usalama vinaendelea kukabiliana na watu hao, Bado haijabainika mara moja iwapo ni tukio la kijambazi ama Kigaidi.

MAGAZETI YA LEO 29.7.2017 TUMEKUSOGEZEA HAPA





















KAFULILA AALIKWA NA MAREKANI KUSHIRIKI MJADALA WA VITA DHIDI YA UFISADI



Serikali ya Marekani imemualika aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila kushiriki kongamano litakaloambatana na ziara ya wiki tatu kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu vita dhidi ya ufisadi litakalofanyika jijini Washington nchini humo.

Kafulila ambaye ameondoka juzi anatarajiwa kurudi nchini agosti 20 mwaka huu, amekuwa mingoni mwa washiriki 12 walioalikwa kutoka barani Afrika ambapo watajifunza pia kuhusu mfumo wa uwazi na uwajibikaji nchini Marekani, mifumo ya manunuzi serikalini, mikakati ya kukabiliana na rushwa serikalini, nafasi za jumuiya za kiraia katika vita dhidi ya ufisadi na mengine mengi.

Kafulila ameuweka wazi uteuzi huo jana ikiwa ni siku chache tangu Rais John Magufuli amsifu kwa kuibua sakata la uchotaji wa zaidi ya shilingi bilioni 300 kwenye akaunti maalum ya Tegeta Escrow.

Akizungumzia uteuzi huo, Kafulila amesema kuwa ingawa watu wengi wanadhani kuwa umetokana na kauli ya Rais John Magufuli, uteuzi huo aliupata kabla ya kauli hiyo na kwamba kauli ya Rais iliongeza baraka juu ya hatua aliyokuwa ameifikia.

“Uteuzi huu ulifanyika kabla ya Mheshimiwa Rais kuzungumza kuhusu mimi. Lakini hata kabla ya hapo, taasisi inayounganisha wanaharakati Tanzania, kupitia chombo chao cha Watetezi wa Watetezi wa Haki za Binadamu walinipa tuzo ya wapiga filimbi (whistle blowers) kwa mchango wangu kwenye vita dhidi ya ufisadi,” amesema Kafulila.

ASKARI WATAKAOWABAMBIKIA KESI WANANCHI KUFUKUZWA KAZI

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amewaonya askari polisi kuacha tabia ya kuwabambikia wananchi kesi huku akiahidi kwatimua kazi watakaobainika kufanya hivyo, anaandika Mwandishi Wetu.

IGP Sirro alisema askari wa aina hiyo ndiyo anaowatafuta na kwamba akiwabaini atawatimua kazi ili kuhakikisha jeshi la polisi linaaminika katika jamii nzima.

Sirro alitoa kauli hiyo alipotoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari baada ya kumaliza shughuli zilizokuwa zimepangwa na jeshi hilo kanda maalum Tarime na Rorya.

Sirro ameonya kwamba askari wa namna hiyo hawatakiwa na kwamba kila mtumishi wa jeshi hilo lazima awe na weledi, amewataka wananchi watakaokumbwa na tatizo hilo kutoa taarifa kwa maofisa wa jeshi hilo ili kuwabaini wale wanaoendekeza tabia hiyo.

”Hizi habari za baadhi ya askari polisi kuendekeza tabia ya kuwabambikia kesi wananchi zinasikika mitaani, hebu wale wanye shida hiyo wawaoneni na kutoa taarifa kwa maafisa wa polisi na kamanda wa kanda maalum Tarime na Rorya ili sisi tuweze kuwashughulikia vilivyo askari polisi wa namna hiyo” alisema Sirro.

Katika hatua nyingine IGP Sirro aliwaondoa hofu waandishi wa habari kwamba watakuwa salama wanapokuwa wanafanya kazi na jeshi hilo na kuwataka kulinda maadili ya kazi yao.


WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS ANAYESHUGHULIKA NA MUUNGANO NA MAZINGIRA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira
January Makamba siku ya jana alikagua mradi ambao unasimamiwa na ofisi yake unaohusisha kujenga kuta kudhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya fukwe mbalimbali nchini.

Ujenzi huo kwa kiasi kikubwa utapendezesha maeneo ya fukwe hizo kwani pia utahusisha ujenzi na uboreshaji sehemu za kupumzikia na kujisomea.

Pichani Waziri Makamba akikagua ujenzi unaoendelea katika eneo la fukwe barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam.







KUSHUKA KWA SARAFU YA NIGERIA YAPUNGUZA UTAJIRI WA ALIKO DANGOTE

KUSHUKA KWA SARAFU YA NIGERIA YAPUNGUZA UTAJIRI WA ALIKO DANGOTE

Bilionea raia wa Nigeria Aliko Dangote ameshuka katika nafasi ya watu tajiri duniani hadi 105 kutoka nafasi ya 51.

Jarida la Forbes limeripoti kwamba mali ya dangote imepungua kutoka dola bilioni 15.4 mwaka 2016 hadi dola bilioni 12.2 mwaka huu kutokana na kushushwa thamani kwa sarafu ya Nigeria.

Dangote alijipatia utajiri wake kupitia uzalishaji wa simiti, sukari, na unga wa ngano.
Aligonga vichwa vya habari 2016 wakati aliposema kuwa alitaka kuinunua Arsenal katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Hapo jana Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos alimpiku Bill Gates kwa muda mfupi kama mtu tajiri duniani kabla ya kushuka hadi nafasi ya pili.

MIZENGWE YA UCHAGUZI MDAU WA SOKA SHAFFIH DAUDA AJIENGUA RASMI

MIZENGWE YA UCHAGUZI: Mdau wa soka nchini ambaye pia ni mwanahabari katika sekta ya michezo, Shaffih Dauda ajiengua rasmi katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa Shirikiso la Soka Nchini (TFF).

“Kutokana na makandokando haya mimi kama  Shaffih Dauda wa maslahi mapana nimeamua kujitoa rasmi kugombea nafasi ya ujumbe wa TFF, Nimetumia muda mrefu kujenga brand yangu hakuna haja kuendelea kung'ang'ania. Suala la rushwa ni kunichafua na mimi sitaki. Kuonyesha uwajibikaji ni jambo jema. Nipo kwenye mfumo wa mpira watu wakikuchafua kwa rushwa ni kuharibu 'future' yako. Mchango wangu kama mdau wa michezo najitahidi sana kuwasaidia vijana kufika mbali kwenye maendeleo ya soka,” ilisema sehemu ya taarifa yake.

Friday, 28 July 2017

JUMUIYA YA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA IMELAANI WAUMINI 10 WA DINI HIYO KUTEKWA WAKIWA KATIKA MSIKITINI

Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania imelaani waumini 10 wa dini hiyo kutekwa wakiwa katika msikiti
wa Ali Mchumo wilayani Kilwa na sasa hawajulikani walipo. Akizungumza leo Alhamisi Julai 27, Katibu wa jumuiya hiyo, Sheikh Ponda Issa Ponda amesema Julai 21, mwaka huu usiku waumini hao wakiwa wanasali katika msikiti huo walivamiwa na watu waliokuwa kwenye magari matano. Amesema wavamizi hao waliingia msikitini na kuanza kuwapiga waumini hao kisha wakaondoka nao. Amesema kabla ya kuingia msikitini, walipiga risasi sehemu mbalimbali za msikiti huo. Ponda amesema wakati wakitekeleza unyama huo, majirani walisikia mayowe ya waumini hao. Amesema baada ya hapo majirani walishuhudia wavamizi hao wakiwa wamewabeba waumini hao na kuwaingiza kwenye magari na kuondoka nao. Amesema baada ya tukio hilo majirani walishuhudia damu nyingi ndani ya msikiti huo. "Sijui kama watu hao watakuwa wazima hadi sasa kwa kuwa waliondoka wakiwa wamebebwa" amesema.

28.07.2017 MAGAZETI YA LEO TANZANIA TUMEKUSOGEZEA HAPA



































Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post