Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Wednesday, 28 June 2017

TUKUKURU INAWASHIKILIA RAIS WA TFF JAMAL MALINZI NA KATIBU MKUU, CELESTINE MWASIGWA

DAR:Rais wa TFF Jamal Malinzi na karibu wake Celestine Mwasingwa waojiwa na polisi.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza kwamba Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi na katibu mkuu wake Celestine Mwesigwa usiku wa kuamkia leo tarehe 28, June, 2016 walikatamatwa na mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini – TAKUKURU na huenda leo wakafikishwa mahakama ya mkazi Kisutu kujibu mashtaka juu ya matumizi mabaya ya ofisi.
Kwa muda mrefu kumekuwepo na tuhuma mbalimbali dhidi yao kuhusu matumizi mabaya ya fedha za Taasisi hiyo ya kitaifa na inasemekana TAKUKURU wamekuwa kwenye uchunguzi dhidi kwa muda sasa mpaka jana walipoamua kuwatiwa nguvuni.
Hivi karibuni gazeti la Nipashe liliandika mfululizo wa makala zilizokuwa zikielezea tuhuma za ufisadi zilielekezwa kwa Malinzi na viongozi wenzake wa TFF.
JAMALI AMEFANYA HAYA UFISADI WA KUTISHA TFF, Ripoti ya ukaguzi wa fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania kwa Taifa Stars iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inaelezwa kuwa, mbali na mambo mengine, TBL iliamua kufanya ukaguzi huo ili kujiridhisha kama shirikisho linazingatia makubaliano yaliyomo kwenye mkataba.
Inaelezwa katika ripoti hiyo ambayo uongozi wa juu wa TBL uliithibitishia Nipashe jana kwamba ilifanywa na Mkaguzi Mkuu wake wa ndani, Richard Magongo, kuwa kati ya Novemba 13, 2013 (siku 11 tangu uongozi wa sasa wa TFF uingie madarakani) na Februari 15, 2014, Dola za Marekani 315,577 (Sh. milioni 688.368) zilitumika bila ya nyaraka za kuthibitisha matumizi yake kinyume cha makubaliano ya mkataba wa pande hizo mbili.
Kati ya Novemba 11, 2013 na Machi 11, 2014, Dola za Marekani 381,248 (Sh. milioni 831.616) pia zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo hazijaanishwa katika mkataba wa TBL na TFF, ripoti inabainisha.
Mchanganuo wa ripoti hiyo unaonesha kuwa, miongoni mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutumia fedha hiyo ni pamoja na rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye Desemba 24, 2013 alilipwa Dola za Marekani 159 kupitia vocha yenye namba 1075 zikiwa ni gharama za malazi hotelini (Hotel accommodation).
Ripoti inaonesha kuwa, siku hiyo hiyo (Desemba 24, 2013), Malinzi alilipwa na TFF Dola 10,000 kupitia vocha namba 1077 (Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya fedha za Jamal Malinzi), kisha Februari 6, 2014 akalipwa Dola 15,934 (Loan Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya mkopo kutoka kwa Jamal Malinzi) na baadaye kulipwa Dola 69,471 kupitia vocha namba 1098 na Dola 63,735 kupitia vocha namba 1401.
Wengine waliopewa fedha hiyo ya udhamini wa TBL kwa Taifa Stars ni aliyekuwa msaidizi wa Malinzi, Juma Matandika, Ali Ruvu na mwingine aliyetajwa kwa jina la S. Madadi ambao kwa pamoja walilipwa Dola 1,084 kupitia vocha namba 828 Februari 6, 2014.
Ripoti pia inabainisha malipo ya Dola 3,500 Januari 16, 2014 kwa ajili ya ziara ya Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF jijini Nairobi.
Pia zimo Dola 4,630 zilizochotwa Desemba 24, 2013 kugharamia mtihani wa utimamu wa mwili kwa waamuzi (Cooper test for referees), Dola 4,120 zilizotolewa siku hiyo hiyo kwa ajili ya Ally Mayay na Ayubu Nyenzi kufanya ziara Uganda na Dola 1,638 ambazo zilitolewa siku hiyo hiyo zikiwa fidia ya malipo ya deni la TFF kulipia ziara ya uongozi wa shirikisho mkoani Mwanza

No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post