Mwenyekiti wa kijiji cha Mangwi kata ya Mchukwi wilayani Kibiti mkoani Pwani Bw. Hamisi Bakari Mkima na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bw. Shamte Rashid Makalaa wa CCM wamefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiofahamika huku Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo kilipo kijiji hicho Bw. Michael Nicolaus (CCM) akinusurika kufa baada ya kujeruhiwa maeneo ya kichwani na kutobolewa macho na wauaji kutokomea mahala pasipojulikana,
Mwenyekiti na afisa wamezikwa leo huko huko kibiti mkoa wa pwani.
Akiongea kwa majonzi mjane wa mwenyekiti Hamisi Bakari alisema kabla watu hao walimuuliza maswali matatu tu marehemu,mke huyo wa marehemu hakuweza kuweka bayana maswali hayo.
No comments:
Post a Comment