Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge imelibebesha Bunge mzigo kuhusu shauri la Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari la kuidharau Mamlaka ya Spika na Bunge baada ya kutopendekeza adhabu kwa mbunge huyo.
Nassari anatuhumiwa kuidharau mamlaka hiyo wakati Bunge lilipokuwa likijadili bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Juni Mwaka jana.
Akisoma mapendekezo ya kamati hiyo leo (Jumatano) mbele ya Bunge, Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika amesema kamati hiyo imemtia hatiani kwa makosa ya kuidharau Mamlaka ya Spika.
"Joshua Nassari aliitika wito wa Kamati bila kuleta usumbufu wa aina yoyote na alipohojiwa na kamati alikiri wazi kosa lake na kuomba radhi kwa Mheshimiwa Spika na Bunge,"amesema.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment