Mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano nchini-TCRA- imeyataka makampuni ya simu kusitisha matangazo ya biashara yanayowekwa kabla ya miito ya simu ili kuwawezesha watumiaji wa simu kupata huduma ya mawasiliano kwa haraka zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari,Mkurugenzi mkuu wa TCRA nchini-TCRA Mhandisi James Mitayakingi Kilaba amesema mamlaka hiyo haiwezi kukubali kuwepo na matangazo ya biashara kabla ya miito ya simu kutoka na kuchelewesha huduma ya mawasiliano ambapo amesisitiza tayari TCRA imeyata makampuni ya simu kukutana kuzungunzia kero hiyo.
No comments:
Post a Comment