Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Monday, 26 June 2017

LOWASSA ATAKIWA OFISI YA UPELELEZI, CHADEMA KUMSINDIKIZA


KADA wa Chadema na aliyepata kuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ametakiwa kuripoti ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini siku ya kesho saa nne asubuhi.
Lowassa ambaye anahusishwa na tuhuma za kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond ya Marekani 2007. Hatua iliyopekea kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri mkuu, amekua lulu kwenye siasa za upinzani kwa sasa.
Hatua hii inahusishwa kupelekwa Mahakamani ambayo imefuata baada ya Serikali kuamua kufuatilia kwa ukaribu tuhuma na kashfa kubwakubwa zilizowahi kutokea katika awamu ya nne na kuwafikisha watuhumiwa mahakamani.
Wengine wanahusisha na kauli yake ambayo imeonekana ya kichochezi ambapo inadaiwa Lowassa aliisihi Serikali kufuata utawala bora na kuitaka kuangalia kwa makini mwenendo wa kesi za masheikhe wa UAMSHO.
Mpaka sasa Waziri huyo mstaafu hajaueleza umaa kama ataitikia wito huo au la! Ingawa taarifa za awali kutoka katika chama chake zimethibitisha wito huo.
Kupitia mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa CHADEMA. Tumaini Makene amedai chama chao kitamsindikiza huku mapema leo wakiwaandaa mawakili wa chama hiko ili kutoa msaada hiyo kesho.
“Tayari Chama kimetoa maelekezo kwa Kurugenzi ya Katiba na Sheria ya Chama kuhakikisha kuwa Mhe. Lowassa anapata msaada wa kisheria wakati wa mahojiano hayo.” alisema Makene
“Taarifa za awali zinaonesha kuwa mahojiano hayo yanahusishwa na kauli za Mhe. Lowassa alizotoa katika nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki futari pamoja na Watanzania wenzetu Waislam waliokuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambapo amekuwa kiitaka Serikali kuzingatia misingi ya utawala bora kama mojawapo ya misingi muhimu ya kuendesha nchi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Watanzania wote.” aliongeza mkuu huyo wa idara.

No comments:

Post a Comment

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post