Latest News

Comments

tanganyika we speak the truth always

Friday, 30 June 2017

KAMA WATANZANIA HAWAJAONGEA KUHUSU VIONGOZI WAO WA KIDINI, NANI ATAONGEA..?Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe, amesema 'Hoja ya Masheikh kukaa miaka mingi bila ya kufikishwa Mahakamani, Serikali isituzibe midomo'. alisema hayo katika clip fupi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mfupi uliopita.

https://youtu.be/8zYzyRJG6xo

MAKAMU MKUU WA SHULE YA SEKONDARI AKUTWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI DARASANI

Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Mkoani Njombe, Ally Kasinge ameagiza kushikiliwa kwa Makamu Mkuu wa shule ya sekondari Wanike, iliyopo katika wilaya hiyo baada ya kukamatwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wake darasani usiku.
Kasinge ametoa agizo hilo baada ya kuwepo taarifa ya kuwepo kwa watu wanaotaka kumsaidia mwalimu huyo kuvuruga ushahidi kwa kupanga na wanafunzi wenye ushahidi huo kuongea tofauti na tukio.
"Kuanzia wanafunzi waliotimuliwa wahojiwe na polisi na wale wanafunzi wengine waliotajwa pia wahojiwe na polisi na mwalimu mwenyewe pia aendelee kushikiliwa .Huyo ambaye anatuhumiwa aendelee kushikiliwa na polisi mpaka tupate majibu, kwa sababu akibaki nje ataendelea kutengeneza mazingira ya kutengeneza mtandao wa kutaka kumsaidia na kupotosha ushaidi"alisema Mkuu wa Wilaya Ally Kasinge
Mbali na hilo shule ya sekondari ya Wanging'ombe pamoja na Wanike zimepandishwa hadhi na sasa zitapokea wanafunzi wa kidato cha tano, walimu wa shule hizo wameweka wazi kuwa shule hizo zinachangamoto ya walimu wa sayansi ambao ni wachache ukilinganisha na walimu wa masomo ya sanaa.
Chanzo: Mpekuzi

TCRA yataka makampuni ya simu kusitisha matangazo yanayowekwa kabla ya miito ya simu


Mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano nchini-TCRA- imeyataka makampuni ya simu kusitisha matangazo ya biashara yanayowekwa kabla ya miito ya simu ili kuwawezesha watumiaji wa simu kupata huduma ya mawasiliano kwa haraka zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari,Mkurugenzi mkuu wa TCRA nchini-TCRA Mhandisi James Mitayakingi Kilaba amesema mamlaka hiyo haiwezi kukubali kuwepo na matangazo ya biashara kabla ya miito ya simu kutoka na kuchelewesha huduma ya mawasiliano ambapo amesisitiza tayari TCRA imeyata makampuni ya simu kukutana kuzungunzia kero hiyo.

Kibiti: Polisi yaua watu wanne(4) wanaodhaniwa kujihusisha na mauaji wilayani humo

Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.
Sabas alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.
"Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji" Alisema Sabas.
Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.
Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
CHANZO: ITV

Wawekezaji Tanzania washtushwa na hatua ya Magufuli

Miswada mitatu itayokayo walazimisha makampuni yanayochimba madini na nishati nchini Tanzania kurekebisha mikataba yao ni hatua ambayo imewashtua wawekezaji wa kigeni.
Miswada mitatu
Miswada mitatu iliwasilishwa na serikali ya Tanzania kwenye Bunge Alhamisi ambayo itairuhusu kuyalazimisha makampuni yanayochimba madini na nishati kufanya mazungumzo juu ya kurekebisha mikataba yao.
Shirika la Habari la Reuters limeripoti kuwa haikufahamika mara moja ni jinsi gani pendekezo la mazungumzo hayo juu ya mikataba litaathiri mradi wa Dola za Marekani bilioni 30 wa gesi, au sekta ya madini iliyoko tayari mashakani, ambayo inaiingizia Tanzania pato la asilimia 3.5 la uchumi wake wa ndani.
Malalamiko ya wafanyabiashara
Wafanyabiashara wamelalamika kuwa wanahisi Rais John Magufuli anawabana pasipo na haki kupitia tafsiri kadamizi za sheria za kodi, ikiwemo ongezeko la faini na madai ambayo wamekuwa wakiyaorodhesha kwa haraka katika soko la hisa la ndani ya nchi.
Lakini Magufuli anasema mageuzi hayo yataongeza uwazi na pato la taifa na kuwa makampuni yamekuwa hayalipi kodi stahili, madai ambayo wao wanayakanusha.
Miswada hiyo inategemewa kufanyiwa kazi haraka na bunge, na itawaathiri makampuni ya kimataifa na itafuatiwa na mapendekezo ya kamati inayofanya uchunguzi wa biashara ya machimbo ya dhahabu inayoendelea katika nchi hii ya Afrika Mashariki.

Thursday, 29 June 2017

RONALDO APATA WATOTO MAPACHA

Mchezaji wa realmadrid na timu ya taifa ya ureno Christian Ronaldo kapata watoto mapacha amekuwa akipata pongezi nyingi kutoka kwa mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Instagram baada ya kuweka picha akiwa amewashika watoto hao na kuandika "so happy to be able to hold the two Love's of my life"

MALINZI NA KATIBU MKUU WA TFF WASOMEWA MASHITAKA 28

UPDATE: Malinzi, Mwesigwa na Nsiana wamesomewa mashtaka 28
Kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa EXCOM imeridhia kubadilishwa kwa Signatories wa Bank hii inamhusu Malinzi na Mwesigwa pia.
Kufoji risiti za kuwa Malinzi anaidai TFF (risiti zipo zaidi 20 zinazodaiwa kufojiwa) hii inamhusu Malinzi pekee.
Na Mwisho ni shtaka la kutakatisha fedha dola za kimarekani 375418 hii inamhusu Malinzi, Mwesigwa na Nsiana

DIWANI WA CHADEMA AJIUZULU KISA ATAKANGAZA KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

ARUSHA: Diwani wa Muriet(CHADEMA) Credo Kifukwe ajiuzulu na kutangaza kumuunga mkono Rais Magufuli.
- Katika maelezo yake amesema "Ninajiuzulu nafasi yangu ili niweze kumuunga mkono Rais Magufuli katika utendaji wake, dhamira inanisuta kuwa katika kundi linalopinga kila kitu"

Wabunge wanawake watengewa chumba maalum cha kunyonyeshea Bungeni

Bunge limetenga chumba maalum kwa ajili ya wabunge wenye watoto wachanga kunyonyesha watoto wao wakati vipindi vya bunge vinaendelea.
Uamuzi huo umetangazwa leo (Jumatano) bungeni na Naibu Spika Dk Tulia Ackson mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni.
"Ofisi ya Bunge inataarifu kuwa imetenga chumba maalum kwa ajili ya kunyonyeshea kwa wabunge wenye watoto wachanga,"amesema.
Amewasihi wabunge wenye watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao angalau miaka miwili kama inavyoshauriwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Chanzo: Mwananchi

Amir wa Dubai asaidia kuwanunulia kanisa wanakijiji

Amir wa Dubai Sheikh Mohammed Bin Rashid Al Maktoum amesaidia kijiji kimoja kidogo kulinunua kanisa dogo la Methodist nchini Uingereza.
Wakaazi wa eneo la Godolphin karibu na Helston walimtumia ujumbe kwa lengo la kufanya mchango.
Kijiji hicho kina jina linalofanana na Godolphin Stables kilichoanzishwa na Sheikh huyo kulingana na Cornwal.
Richard Mackie kutoka muungano wa jamii ya Godolphin Cross alisema: Tunamshukuru sana.
Kundi hilo lilihitaji pauni 90,000 kulinunua kanisa hilo ambalo walitaka kulibadilisha na kulifanya kituo cha jamii na walikuwa wamechangisha pauni 25,000.
Haijulikani ni kiwango gani cha fedha kilichotolewa na Sheikh Mohammed ,lakini Mackie alisema ''ametusaidia sana''.
Mwanakijiji mmoja Valerie Wallace alikuwa na wazo hilo kama hatua ya mwisho baada ya kundi hilo kushindwa kuchangisha fedha kutoka maeneo mengine.
''Hatukufikiria wazo kama hilo lakini baadaye tukaanza kupata simu kutoka Abu Dhabi, bwana Mckie alisema. Tulidhani tulikuwa tunafanyiwa mzaha lakini baadaye tukagundua sio kwamwe''. 
CHANZO:BBC 

Wednesday, 28 June 2017

MWENYEKITI WA KIJIJI NA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI WA CCM WAUWAWA KIBITI


Mwenyekiti wa kijiji cha Mangwi kata ya Mchukwi wilayani Kibiti mkoani Pwani Bw. Hamisi Bakari Mkima na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bw. Shamte Rashid Makalaa wa CCM wamefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiofahamika huku Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo kilipo kijiji hicho Bw. Michael Nicolaus (CCM) akinusurika kufa baada ya kujeruhiwa maeneo ya kichwani na kutobolewa macho na wauaji kutokomea mahala pasipojulikana,
Mwenyekiti na afisa wamezikwa leo huko huko kibiti mkoa wa pwani.
Akiongea kwa majonzi mjane wa mwenyekiti Hamisi Bakari alisema kabla watu hao walimuuliza maswali matatu tu marehemu,mke huyo wa marehemu hakuweza kuweka bayana maswali hayo.

Bunge lashindwa kutoa adhabu kwa Nassari

Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge imelibebesha Bunge mzigo kuhusu shauri la Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari la kuidharau Mamlaka ya Spika na Bunge baada ya kutopendekeza adhabu kwa mbunge huyo.
Nassari anatuhumiwa kuidharau mamlaka hiyo wakati Bunge lilipokuwa likijadili bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Juni Mwaka jana.
Akisoma mapendekezo ya kamati hiyo leo (Jumatano) mbele ya Bunge, Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika amesema kamati hiyo imemtia hatiani kwa makosa ya kuidharau Mamlaka ya Spika.
"Joshua Nassari aliitika wito wa Kamati bila kuleta usumbufu wa aina yoyote na alipohojiwa na kamati alikiri wazi kosa lake na kuomba radhi kwa Mheshimiwa Spika na Bunge,"amesema.
Chanzo: Mwananchi

TUKUKURU INAWASHIKILIA RAIS WA TFF JAMAL MALINZI NA KATIBU MKUU, CELESTINE MWASIGWA

DAR:Rais wa TFF Jamal Malinzi na karibu wake Celestine Mwasingwa waojiwa na polisi.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza kwamba Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi na katibu mkuu wake Celestine Mwesigwa usiku wa kuamkia leo tarehe 28, June, 2016 walikatamatwa na mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini – TAKUKURU na huenda leo wakafikishwa mahakama ya mkazi Kisutu kujibu mashtaka juu ya matumizi mabaya ya ofisi.
Kwa muda mrefu kumekuwepo na tuhuma mbalimbali dhidi yao kuhusu matumizi mabaya ya fedha za Taasisi hiyo ya kitaifa na inasemekana TAKUKURU wamekuwa kwenye uchunguzi dhidi kwa muda sasa mpaka jana walipoamua kuwatiwa nguvuni.
Hivi karibuni gazeti la Nipashe liliandika mfululizo wa makala zilizokuwa zikielezea tuhuma za ufisadi zilielekezwa kwa Malinzi na viongozi wenzake wa TFF.
JAMALI AMEFANYA HAYA UFISADI WA KUTISHA TFF, Ripoti ya ukaguzi wa fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania kwa Taifa Stars iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inaelezwa kuwa, mbali na mambo mengine, TBL iliamua kufanya ukaguzi huo ili kujiridhisha kama shirikisho linazingatia makubaliano yaliyomo kwenye mkataba.
Inaelezwa katika ripoti hiyo ambayo uongozi wa juu wa TBL uliithibitishia Nipashe jana kwamba ilifanywa na Mkaguzi Mkuu wake wa ndani, Richard Magongo, kuwa kati ya Novemba 13, 2013 (siku 11 tangu uongozi wa sasa wa TFF uingie madarakani) na Februari 15, 2014, Dola za Marekani 315,577 (Sh. milioni 688.368) zilitumika bila ya nyaraka za kuthibitisha matumizi yake kinyume cha makubaliano ya mkataba wa pande hizo mbili.
Kati ya Novemba 11, 2013 na Machi 11, 2014, Dola za Marekani 381,248 (Sh. milioni 831.616) pia zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo hazijaanishwa katika mkataba wa TBL na TFF, ripoti inabainisha.
Mchanganuo wa ripoti hiyo unaonesha kuwa, miongoni mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutumia fedha hiyo ni pamoja na rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye Desemba 24, 2013 alilipwa Dola za Marekani 159 kupitia vocha yenye namba 1075 zikiwa ni gharama za malazi hotelini (Hotel accommodation).
Ripoti inaonesha kuwa, siku hiyo hiyo (Desemba 24, 2013), Malinzi alilipwa na TFF Dola 10,000 kupitia vocha namba 1077 (Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya fedha za Jamal Malinzi), kisha Februari 6, 2014 akalipwa Dola 15,934 (Loan Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya mkopo kutoka kwa Jamal Malinzi) na baadaye kulipwa Dola 69,471 kupitia vocha namba 1098 na Dola 63,735 kupitia vocha namba 1401.
Wengine waliopewa fedha hiyo ya udhamini wa TBL kwa Taifa Stars ni aliyekuwa msaidizi wa Malinzi, Juma Matandika, Ali Ruvu na mwingine aliyetajwa kwa jina la S. Madadi ambao kwa pamoja walilipwa Dola 1,084 kupitia vocha namba 828 Februari 6, 2014.
Ripoti pia inabainisha malipo ya Dola 3,500 Januari 16, 2014 kwa ajili ya ziara ya Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF jijini Nairobi.
Pia zimo Dola 4,630 zilizochotwa Desemba 24, 2013 kugharamia mtihani wa utimamu wa mwili kwa waamuzi (Cooper test for referees), Dola 4,120 zilizotolewa siku hiyo hiyo kwa ajili ya Ally Mayay na Ayubu Nyenzi kufanya ziara Uganda na Dola 1,638 ambazo zilitolewa siku hiyo hiyo zikiwa fidia ya malipo ya deni la TFF kulipia ziara ya uongozi wa shirikisho mkoani Mwanza

Monday, 26 June 2017

LOWASSA ATAKIWA OFISI YA UPELELEZI, CHADEMA KUMSINDIKIZA


KADA wa Chadema na aliyepata kuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ametakiwa kuripoti ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini siku ya kesho saa nne asubuhi.
Lowassa ambaye anahusishwa na tuhuma za kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond ya Marekani 2007. Hatua iliyopekea kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri mkuu, amekua lulu kwenye siasa za upinzani kwa sasa.
Hatua hii inahusishwa kupelekwa Mahakamani ambayo imefuata baada ya Serikali kuamua kufuatilia kwa ukaribu tuhuma na kashfa kubwakubwa zilizowahi kutokea katika awamu ya nne na kuwafikisha watuhumiwa mahakamani.
Wengine wanahusisha na kauli yake ambayo imeonekana ya kichochezi ambapo inadaiwa Lowassa aliisihi Serikali kufuata utawala bora na kuitaka kuangalia kwa makini mwenendo wa kesi za masheikhe wa UAMSHO.
Mpaka sasa Waziri huyo mstaafu hajaueleza umaa kama ataitikia wito huo au la! Ingawa taarifa za awali kutoka katika chama chake zimethibitisha wito huo.
Kupitia mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa CHADEMA. Tumaini Makene amedai chama chao kitamsindikiza huku mapema leo wakiwaandaa mawakili wa chama hiko ili kutoa msaada hiyo kesho.
“Tayari Chama kimetoa maelekezo kwa Kurugenzi ya Katiba na Sheria ya Chama kuhakikisha kuwa Mhe. Lowassa anapata msaada wa kisheria wakati wa mahojiano hayo.” alisema Makene
“Taarifa za awali zinaonesha kuwa mahojiano hayo yanahusishwa na kauli za Mhe. Lowassa alizotoa katika nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki futari pamoja na Watanzania wenzetu Waislam waliokuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambapo amekuwa kiitaka Serikali kuzingatia misingi ya utawala bora kama mojawapo ya misingi muhimu ya kuendesha nchi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Watanzania wote.” aliongeza mkuu huyo wa idara.

AFRIKA KUSINI:Wakulima wawili watafikishwa mahakamani, tuhuma za kumuingiza ndani ya jeneza raia mweusi akiwa hai

Wakulima wawili weupe watafikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini , baada ya kutuhumiwa kuwa walimsukuma mtu mmoja mweusi na kumuingiza ndani ya jeneza, huku wakitishia kumwagia mafuta ya petroli na kumteketeza moto, akiwa hai.

_96680699_d63fd1bc-09d8-4ead-ab7c-3ca96af434a7.jpg

Wakati Victor Mlotshwa alipokataa, wakulima hao walimtishia kuwa watamweka ndani ya jeneza hilo pamoja na nyoka.

Washtakiwa hao Willem Oosthuizen na Theo Jackson, walikamatwa mwezi Novemba mwaka jana, baada ya video ya kitendo hicho kilipowekwa mitandaoni.

Walisema kuwa, Bwana Mlotshwa alipitia kwenye shamba lao liliko katika jimbo la Mpumalanga, bila ya kuwa na idhini, na walikuwa wakimuadhibu.

Katika kusikizwa kwa kesi hiyo awali, jaji wa mahakama alisema kuwa wakulima hao walikuwa wakatili na waliojaa tabia za ubaguzi wa rangi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin anyeshewa na Mvua Wakati wa Sherehe ya Umma

Rais wa Urusi Vladimir Putin aliingia ndani ya Moscow wakati wa sherehe ya kukumbuka uvamizi wa Nazi wa Urusi wakati wa Vita Kuu ya Pili. Rais alisimama peke yake katika mvua ya joto akitazama kimya kwenye kodi ya maua mnamo Juni 22, pia anajulikana kama Siku ya Kumbukumbu na Mshangao, ambayo inaonyesha wakati Hitler alipomaliza kushikamana na Stalin.
Jitihada za Kirusi za kuacha Blitzkrieg ya Nazi na kuimarisha wilaya iliyopotea hatimaye ilikuwa na maisha ya watu milioni 26, ikiwa ni pamoja na wananchi wengi ambao walipata njaa. Matukio ya kukumbuka jukumu la Urusi na dhabihu katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia imechukua umuhimu maalum chini ya utawala wa Putin, ambayo inategemea kiburi cha kitaifa kuimarisha umaarufu wake na kumtia nguvu.
Wakati wengi katika umati walibeba miavu kwa tukio hilo, Putin alionekana kuwa anachagua kwenda bila, badala yake akasimama mbele ya mvua kali. Dmitry Medvedev, Waziri Mkuu, pia alikwenda bila makazi. Wale wawili hatimaye walitolewa na marufuku walipokuwa wakiangalia jeshi la kijeshi katika Alexander Garden, pamoja na ukuta wa Kremlin, ambapo kumbukumbu iko.

MBUNGE MNYIKA ALIVYOTOLEWA NA POLISI BUNGENI

Recent in Sports

3/MICHEZO/post-grid

Recent Post